Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, akizungumza katika uzinduzi
wa mradi wa kuunganisha umeme kati ya Kenya na nchi Tanzania.
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania Mkoa wa Arusha (Tanesco ), Herrin Mhina, akitoa maelezo ya mradi mbele ya mgeni rasmi.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Murro, akizungumza katika uzinduzi huo wa mradi wa kuunganisha umeme Kenya na Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha akioneshwa mchoro wa mradi huo na mkandarasi
wa mradi wa kuunganisha umeme kenya na Tanzania mkandarasi m/s Gopa
kutoka International Enegy Consultant GmbH kutoka ujerumani.
Na Ahmed Mahmoud, Arusha
Zaidi
ya dola za kimarekani USD 258.82 milioni zinatarajiwa kutumika katika
mradi wa kuunganisha umeme kati ya nchi za Kenya na Tanzania ,ambapo mradi
huu utahusisha ujenzi wa laini kubwa ya msongo wa kilovolti 400 kutoka
Singida kupitia Manyara na upande wa Arusha kwa upande wa Tanzania hadi
Isinya kwa upande wa Kenya.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano kwa mkandarasi wa ujenzi huo meneja wa shirika
la umeme Tanzania mkoa wa Arusha (Tanesco ), Herrin Mhina, alisema kuwa
mradi huu ni mkubwa wa kimkakati wa serikali na laini hii itakuwa na
urefu wa kilometa 510.7 ambapo kilometa 414.7ni kwa upande wa Tanzania
yaani ya Singida na Namanga na kilometa 96 ni kwa upande wa kenya
itakayo toka Namanga hadi Isinya.
Alisema
sambamba na ujenzi wa laini pia mradi utahusisha upanuzi wa vituo vya
kupooza umeme vya dodoma na singida pamoja ujenzi wa kituo kipya cha
kupooza umeme chenye uwezo wa kilovolti 400 kinachojengwa Arusha katika
kijiji cha Lemgur ,aidha pia mradi huu utahusisha usambazaji wa umeme
vijijini ambapo jumla ya vijiji 22 vilivyopo kandokando ya mradi
vitanufaika kwa kuunganishiwa umeme wa msongo wa 33kV vikiwemo vijiji
tisa vilivyopo ndani ya mkoa wa Arusha .
Alisema
kuwa malengo makuu ya mradi ni kuongeza uwezo wa kusafirisha umeme
kwenye gridi yetu ya taifa kufikia kiwango cha juu cha 2000MW pia mradi
huu utasaidia kuwezesha upatikanaji wa umeme wa uhakika na kwa bei nafuu
kuelekea uchumi wa kati na Tanzania ya viwanda pia mradi huu
utawezesha nxhi moja kuweza kuuza umeme kwa nchi nyingine kwa bei nafuu
pindi itakapotokea uhitaji hivyo kusaidia kukuza undugu na ushirikiano
uliopo baina ya nchi ya kenya na Tanzania.
"mradi
huu unatarajiwa kukamilika ifikapo april 2020 ambapo gharama za mradi
zimekadiriwa kuwa USD 258.82milioni kati ya hizo USD 214.93ni fedha za
mkopo toka AfDB na JICA na USD 43.89 milioni zikiwa ni fedha kutoka
ndani"alisema Mhina
Akizindua
rasmi ujenzi wa mradi huo mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo
alipongeza serikali kwa kuwaletea mradi huu kwani huu utachangia
kuimarisha uwezo wa usambazaji wa umeme kwa wananchi na katika nchi zote
mbili na katika eneo la Afrika mashariki kwa ujumla pia zitasaidia
kuondoa baadhi ya gharama za uzalishaji wa umeme wa kutumia mafuta
mazito na gesi kwa kutumia umeme wa maji ambayo itasaidia kupunguza
uzalishaji wa hewa ya ukaa.
Alibainisha
kuwa mradi huu pia umekuja na faida kwani umepita katika kijiji cha
Lemgur na umewasaidia wananchi hao kupata umeme wa uhakika pia wananchi
wa kijiji hicho watanufaika na barabara ambayo ni sehemu ya ujenzi wa
kituo cha kupooza umeme pia mradi huu utasaidia kuondoa changamoto kubwa
ambayo ilikuwa inawakabili wananchi wa eneo hili,na waanchi wa wote
ambao awana umeme watapata.
Msipeane
umeme kwa urafiki,wala kujuana tutafatilia ugawaji wa umeme huu na
umeme huu usitolewe kwa kujuana maana huu mradi ni kwaajili ya
wananchi"alisema Gambo
Aliwasihi
wananchi kuacha nafasi ya kupitisha barabara na mitaro ili shughuli za
maendeleo ziweze kuja kwa urahisi kwani kukiwa na barabara ni rahisi
shughuli za maendeleo kufanyika kiurahisi .
Nae
mkuu wawilaya ya Arumeru Jerry Muro alitumia mda huo kuwaomba
wakandarasi hao kuwapatia vijana wa eneo hilo ajira vijana kwani kuna
vijana wengi wa eneo hilo wenye nguvu na weledi aidha aliwasihi vijana
wa eneo hilo iwapo watapatiwa ajira wafanye kazi kwa nizamu ,weledi,na
wasiwe wadokozi kwani iwapo kijana yoyote ataajiriwa alafu akafanya
udokozi au utovu wa nithamu wa aina yoyote hatua kali zitachukuliwa
dhidi yake.
Naye
mkandarasi wa mradi huo mkandarasi m/s Gopa kutoka International Enegy
Consultant GmbH kutoka ujerumani alisema katika mradi huo changamoto
inayowakabili ipo katika ujenzi wa barabara ambapo usanifu wa barabara
ulilenga kuwa na barabara yenye viwango sawa na barabara za TARURA
ambazo zinaupana usiopungua mita 15 kutoka katika barabara hivyo
kuwezesha kuwepo na mitaro ya maji ambayo sio muhimu tu kwakuilinda
barabara balilakini pia kuzuia maji kufikakwenye makazi ya watu .
"Atukuweza
kupata eneo la kutosha kwa kuwa sehemu nyingi wananchi wamejenga
uziomashamba na hata nyumba ,hivyo changamoto kubwa ni kupata eneo la
kujenga mitaro ya maji yenye kukithi usanifu wa awali" .
No comments:
Post a Comment