NCHI wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zimejipanga kufukia viwanda vinavyoendeshwa kwa mfumo wa kiteknolojia kuanzia mwaka 2021 hadi 2050 ili kuongeza thamani ya bidhaa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Viwanda na Ushindani Sekretarieti ya SADC, Dk. Johansein Rutaihwa wakati akizungumza na Habari Mseto Blog.
Dk. Rutaihwa alisema mwaka 2015 viongozi wa SADC walipokutana nchini Enswatin na kupitisha maazimio ya mkakati wa maendeleo ya viwanda wa 2015 hadi 2063 na kuweka lengo la kuelekea viwanda vya teknolojia na kuondoka katika viwanda vya kutumia rasilimali zaidi.
Alisema iwapo nchi zitaondoka katika viwanda vya kuuza rasilimali kama maharage, korosho, mahindi na mazao mengine uchumi utakuwa kwa haraka kutokana na thamani kuongezeka.
"Viongozi wa SADC waliweka mkakati wenye malengo matatu ikiwemo wa kutoka viwanda vya rasilimali kwenda vya teknolojia ili thamani ya bidhaa itaongezeka hivyo kuanzia mwaka 2021 utekelezaji unaanza," alisema.
Mkuu huyo wa kitengo alisema matarajio yao ni kuona nchi za SADC zinatumia miaka 20 kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya viwanda ili kukuza uchumi wa nchi zao.
Alisema lengo la tatu lililopo katika mkakati huo viwanda vinafikia teknolojia ya kutumia roboti kwa kila kazi na sio kutumia binadamu.
Dk.Rutaihwa alisema malengo hayo mawili yanatekelezwa baada ya nchi wanachama wanachama kuandaa mazingira awamu ya kwanza ya mkakati ni kuandaa mazingira rafiki.
Mkuu huyo alisema katika eneo hilo walikubaliana nchi wanachama zihakikishe mchango wa sekta ya viwanda kwenye unakuwa kwa asilimia 7 ila Tanzania pekee ndio imefanikiwa katika eneo hilo.
Alisema wanataka kutumia mkutano huo wa 39 wa SADC wananchi wa nchi zote hasa wajasiriamali na wenye viwanda kuonesha ni bidhaa gani wanazalisha ndani ya nchi zao.
Aidha alisema kupitia maonesho hayo wadau watapata nafasi ya kutembelea viwanda mbalimbali kujifunza na kuona teknolojia zinazotumika.
Mkuu huyo aliwataka Watanzania kuendelea kujisajili kwa njia ya kieletroniki na kawaida kujisajili waweze kushiriki onesho hilo la aina yake.
Alisema hadi sasa zaidi ya wa watu 370 wamejisajili kushiriki wiki ya viwanda ambapo washiriki wengi wanatoka nje hivyo amewataka Watanzania kutumia fursa hiyo kujitangaza.
No comments:
Post a Comment