Mwenyekiti wa Kijiji cha Shebomeza, Hamisi Barua (kushoto), akiwa na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Amani, Hadija Nassoro, alizungumza na waandishi wa habari wilayani Muheza mkoani Tanga akizungumzia changamoto ya bei ya zao la Msambu.
NA SULEIMAN MSUYA
NA SULEIMAN MSUYA
SERIKALI imeombwa
kufanya utafiti wa zao la Msambu ambalo linapatikana katika Hifadhi ya
Mazingira Asili Amani kata ya Amani wilaya ya Muheza mkoani Tanga.
Ombi hilo limetolewa na
viongozi wa Kijiji cha Shebomeza, kata ya Amani wilaya ya Muheza mkoani Tanga
wakati wakizungumza na Habari Mseto Blog hivi karibuni.
Akizungumzia zao hilo
Mtendaji wa Kijiji cha Shebomeza, Macheal Siafu alisema zao hilo ambalo
linatajwa kupatikana Amani pekee halijanufaisha wananchi hivyo waanamini utafiti
ukifanyika bei yake itaongezeka.
Siafu alisema zipo
kampuni zinafika kikijiji hapo na kununua Msambu lakini kwa uchunguzi wao wa
kawaida wanahisi kuwa bei ambayo inatolewa haiendani na soko la dunia.
“Tunaomba Serikali
ilete watafiti waweze kufanya utafiti ili zao hili liweze kujulikana thamani
yake halisi ambayo itaondoa hofu walionayo wakulima wanaojihusisha na kilimo
hicho,”alisema.
Alisema taarifa walizonazo
ni kwamba zao hilo linalopatikana Amani pekee, linatoa mafuta ambayo yanatumika
kwa chakula na kutengeneza vanilla.
Siafu alisema zipo
taarifa kuwa wapo wanunuzi wanatoka kutoa shilingi 1,500 kwa kilo ila wapo
viongozi wengine wanalazimisha iiuzwe shilingi 600 hadi 800.
Alisema zao hilo
linakubali katika Ukanda wote wa Hifadhi ya Amani hivyo kukiwa na mpango
madhubuti wa kusimamia zao hilo litaongeza mapato ya kijiji, kata, tarafa,
wilaya, mkoa na nchi kwa ujumla.
Mtendaji huyo
alisisitiza kuwa mazao ambayo hayajulikani yamekuwa na uhitaji mkubwa hivyo ni
wakati muafaka kufanyika kwa tafiti ambazo zitasaidia nchi kuongeza kipato.
Ofisa Mtendaji Kata ya
Amani, Hadija Nassoro alisema iwapo jitihada zitaelekezwa katika kukuza na kuongeza
thamani ya zao hilo wananchi wajipatia kipato na kufanya shughuli za maendeleo.
Nassoro alisema
wananchi wake wamekuwa wakijisghulisha na shughuli za maendeleo lakini wakati
mwingine wanakatishwa tama kutokana na bei za mazao yao.
Kaimu Mhifadhi Mkuu wa
Hifadhi ya Amani, Bob Matunda alisema zao la Msambu limekuwa na mchango mzuri
katika uchumi wa wananchi wa Amani na kwamba utafiti ni muhimu ili kujua
thamani ya zao hilo adimu.
Tafiti zinaonesha kuwa
Msambu unapatikana hapa Amani pekee naamini tafiti zinahitajika kufanyika ili
kujua thamani yake kwani inaweza kuongeza thamani ya wakulima.
No comments:
Post a Comment