NA SULEIMAN MSUYA
UAMUZI wa Serikali
kuzuia uvunaji viumbe hai wakiwemo Wadudu aina ya Vipepeo katika Kijiji cha
Shebomeza, Kata ya Amani Wilayani Muheza mkoani Tanga umetajwa kusababisha
umaskini kijijini hapo.
Hayo yamesemwa na
viongozi wa kijiji cha Shebomeza na Kata ya Amani wakati wakizungumza na
Blog hii hivi karibuni.
Mwenyekiti wa Kijiji
cha Shebomeza, HamisI Barua alisema mradi wa Vipepeo ulianza kuleta mabadiliko
ya maisha ya wananchi wake kwa kupata kipato kinachokidhi mahitaji yao.
Barua alisema Kipepeo
alikuwa anaingiza kipato kuliko hata mfugaji ambapo kiwango kidogo mfugaji
alikuwa anaingiza zaidi ya shilingi 500,000.
“Mimi kama Mwenyekiti
wa kijiji nadiriki kusema kuwa uamuzi wa Serikali hauna tija kwa wananchi kwani
ufugaji wa Vipepeo hauna athari kwa mazingira na viumbe hao kwa kuwa utaratibu
unafuatwa,” alisema.
Alisema kutokana na
uamuzi huo wananchi wengi wameshindwa kushiriki kuchangia huduma za kijamii kwa
kukosa kipato.
Mwenyekiti huyo alisema
Vipepeo wana soko kubwa nje ya nchi hivyo ni lazima Serikali kutafakari upya
ili wananchi waweze kuendelea na uzalishaji wa viumbe hao.
Mtendaji wa Kijiji cha
Shebomeza, Michael Siafu, alisema Serikali inapaswa kuja na majibu ya kitafiti
ni hasara gani wamepata kutokana na ufugaji huo wa Vipepeo ndi watoe maamuzi.
Ofisa Mtendaji wa Kata Amani,
Hadija Nassoro (pichani), alisema uamuzi wa Serikali kuzuia ufugaji na uuzaji wa Vipepeo
ulikuwa wa haraka hali ambayo inachangia jamii kurejea katika maisha ya
kusubiri misaada wakati walianza kujikomboa kiuchumi.
“Mimi na ugeni wangu
lakini naona ni vizuri Serikali ikajitafakari umpya kwani Vipepeo huwa
vinazalishwa ndani ya uzio maalumu na ni lazima mazingira yawe mazuri ndio
wanazaliana,” alisema.
Meneja
Mradi wa
Vipepeo, kutoka Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG),
Amir Said alisema kimsingi uamuzi wa Serikali kuzuia biashara hiyo
hauna faida kwa nchi wala wananchi na kusisitiza kuwa miradi
inayoibuliwa
vijijini haina dhamira ya kuharibu mazingira.
“Tumewafundisha
wananchi namna ya kuzalisha vipepeo kwa kutumia eneo dogo ambapo wanawrka nyavu
na uchumi wa wananchi ulianza kuimarika,” alisema.
Jana akijibu maswali ya
viongozi na wananchi wa vijiji vinazalisha Vipepeo Mkuu wa Mkoa wa Tanga,
Martin Shegela aliwataka wananchi hao kuwa na subira wakati Serikali inaendelea
na mchakato utakaotoa majibu sahihi ya nini kifanyike.
No comments:
Post a Comment