Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan akisalimina na Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa hapa Nchini
Bw. Alvaro Rodriguez wakati Bw. Alvaro alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais
Ikulu Jijini Dar Es Salaam leo Agost 21,2019 kwa ajili ya kumuaga Makamu wa
Rais baada ya kumaliza kipindi chake cha Uwakilishi hapa nchini.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa hapa nchini, Alvaro Rodriguez wakati alipofika ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kumuaga Makamu wa Rais baada ya kumaliza kipindi chake cha uwakilishi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali ya Tanzania itaendelea kuunga mkono mageuzi ya mfumo wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa kwenye maeneo mbalimbali yaliyoafikiwa.

Amesema Tanzania itaendelea na mpango wa pili wa Maendeleo
wa Msada wa Umoja wa mataifa ambao unatekelezwa sambamba na Dira ya Zanzibar ya
2020 pamoja na awamu ya pili ya mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa Taifa
(F2016,2021 FYDP2) wenye lengo la kuisaidia Tanzania kufikia Uchumi wa kati
ifikapo Mwaka 2025.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo Agost 21, 2019 Ofisini
kwake Ikulu Jijini Dar Es Salaam wakati alipokutana na kufanya Mazungumzo na
Bw. Alvaro Rodriguez Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa ayefika Ofisini kwake kwa ajili ya kumuaga Baada ya kumaliza kipindi
chake cha Uwakilishi hapa Nchini.
Aidha Makamu wa Rais amemshukuru Bw. Alvaro kwa Ushirikiano
na Uhusiano Mzuri alioujenga baina ya Tanzani na Umoja wa Mataifa katika
kipindi chake chote alichokuwepo hapa Nchini kwa kusukuma Agenda za Nchi na kuiletea mafaniko katika Sekta mbalimbali
na kumtakia kila la heri na kazi njema katika kituo chake kipya cha kazi,
ambapo Bw. Alvaro ameteuliwa kuwa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini
Uturuki.
Wakati huo huo Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa Nchini
Bw. Alvaro ameipongeza Serikali ya
Tanzania kwa kuwasilisha Taarifa za mapitio ya Hiyari (VNR) ya Utekelezaji wa Maelengo ya Maendeleo
Endelevu ya Mwezi Julai 2019 kwa kuwainisha Mafanikio, Changamoto na mbinu bora
za kukabiliana nazo pamoja na kujifunza.
No comments:
Post a Comment