HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 01, 2019

BENKI YA CRDB NA KAULI MBIU YA “KILIMO CHETU, VIWANDA VYETU, UCHUMI WETU” MAONYESHO YA NANE NANE SIMIYU

Benki ya CRDB imeendelea kudhihirisha kuwa Benki kinara katika kuwezesha sekta mbalimbali za maendeleo nchini ambapo katika maonesho ya mwaka huu ya nane nane ambayo kitaifa yanaadhimishwa mkoani Simiyu Benki hiyo imekuja na kauli mbiu ya “Kilimo chetu, Viwanda vyetu, Uchumi wetu”.

Akizungumza katika maonesho hayo ambayo yamezinduliwa rasmi leo hii na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Mkurugenzi wa Wateja wa Kati na Wadogo wa Benki ya CRDB, Boma Raballa, alisema Benki ya CRDB inaamini kuwa uwezeshaji wa sekta ya kilimo utasaidia kuongeza malighafi katika viwanda nchini na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.

“Tukiwa Benki ya kizalendo nchini tupo tayari kushirikiana na Serikali yetu kujenga uchumi wa kati unaoshamirishwa na viwanda. Ambavyo kwa uhalisia vinategemea sana mazao ya kilimo kama malighafi zake,” alisema ndugu Boma Raballa.

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuwa mstari wa mbele kuwezesha sekta ya kilimo kupitia huduma na bidhaa mbalimbali inazozitoa Benki hiyo kwa ajili ya kilimo ikiwamo mikopo ya pembejeo za kilimo.

"Nimefurahishwa sana na kauli mbiu yenu ya 'Kilimo Chetu, Viwanda Vyetu, Uchumi wetu' hii inaonyesha ni jinsi gani Benki hii imejipanga vilivyo kuboresha sekta hii muhimu ambayo ni kichocheo kikubwa katika kufikia uchumi wa kati wa viwanda", alisema Hussein Bashe.

Akimueleza Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe juu ya mchango wa Benki ya CRDB katika maendeleo kilimo nchini ndugu Boma Raballa alisema Benki ya CRDB inatoa zaidi ya asilimia 40% ya mikopo yote itolewayo kwa ajili ya kilimo nchini.

Ambapo kwa kipindi cha mwaka 2018/2019, zaidi ya shilingi bilioni 650 zimeshatolewa. Katika hizo, shilingi bilioni 150 yaani asilimia 23% , zimeelekezwa katika kilimo cha mazao ya biashara na malighafi za viwanda, utengenezaji wa pembejeo, usindikaji na usambazaji.

Raballa alisema pia Benki ya CRDB imekuwa ikishirikiana na kwa karibu wadau wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo nchini ikiwamo Benki Kuu ya Tanzania, Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Shirika la Uwezeshaji wa Kilimo (PASS), Mfuko wa Afrika Gurantee (AGF), Shirika la Uwezeshaji Kifedha la Kimataifa (IFC), Benki ya Maendeleo Afrika (AFDB), Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), Ushirikiano wa Maendeleo ya Viwanda (IDC) na Kampuni ya ETC Agro katika kuwawezesha wakulima nchini kupitia mafunzo mbalimbali juu ya ufahamu wa masuala ya fedha, uwekezaji , utafutaji masoko na mikopo ya kilimo.
Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Wateja wa Kati na Wadogo wa Benki ya CRDB, Boma Raballa wakati alipotembelea banda la Benki ya CRDB katika maonyesho ya 26 ya kilimo na mifugo (Nane Nane 2019), yaliyofunguliwa rasmi leo na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kwenye viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea banda la Benki ya CRDB katika maonyesho ya 26 ya kilimo na mifugo (Nane Nane 2019),  yaliyofunguliwa rasmi leo na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan kwenye viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu. Katikati ni Mkurugenzi wa Wateja wa Kati na Wadogo wa Benki ya CRDB, Boma Raballa.
 Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, akisalimiana na Afisa Masoko Mwandamizi wa Benki ya CRDB, Nassib Kalamba wakati alipotembelea banda la Benki ya CRDB katika maonyesho ya 26 ya kilimo na mifugo (Nane Nane 2019), katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu.
 Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, akizungumza na Meneja wa Biashara wa Benki ya CRDB, Felix Kisenha, wakati alipokuwa akipatiwa huduma za kibenki katika Tawi la Benki ya CRDB linalotembea, katika maonyesho ya 26 ya kilimo na mifugo (Nane Nane 2019), katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu.
 Afisa wa Benki ya CRDB, Maregesi Shaaban akieleza jambo kuhusu huduma ya Malkia Akauti kwa baadhi ya wateja wa Benki hiyo waliotembelea banda lao, wakati wa maonyesho ya 26 ya kilimo na mifugo (Nane Nane 2019), katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu.













No comments:

Post a Comment

Pages