Afisa
Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati Benki ya NMB - Filbert Mponzi
akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa kutangaza
matokeo ya hati
fungani ya Benki hiyo katika ofisi za NMB jana jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa NMB - Ruth Zaipuna.
Afisa Mkuu wa Fedha, Ruth Zaipuna, akizungumza
wakati wa mkutano na waandishi wa habari
wa kutangaza matokeo ya hati fungani ya Benki hiyo katika ofisi za NMB
jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mkuu wateja wadogo na wakati (Chief Retail Banking), Filbert Mponzi
na Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko ya Fedha (Head, Global Markets Treasury department), Gladness Deogratius.
Na Mwandishi Wetu
BENKI
ya NMB, imetangaza matokeo ya mauzo ya toleo la tatu la programu ya hati
fungani ya benki hiyo, ambako imekusanya Sh. Bilioni 83.3 sawa na asilimia 333
ya mauzo yaliyotarajiwa awali ya Sh. Bilioni 25.
Mauzo
ya toleo la tatu la hati fungani ya NMB yalifunguliwa Juni 10 na kufungwa Julai
8, mwaka huu, ambako kipindi hicho cha miezi miwili, kilikuja baada ya Mamlaka
ya Masoko na Mitaji na Dhamana (CMSA), kutoa idhini ya mauzo hayo.
Akizungumza
katika hafla ya kutangaza matokeo hayo, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana,
Afisa Mkuu wa Fedha , Ruth Zaipuna, alisema wao kama benki wanajivunia kiwango
hicho cha mauzo, kinachothibitisha imani ya wananchi na jamii kwa benki yake.
Zaipuna
alibainisha kuwa, tayari NMB imeyapokea na kuyakubali maombi yote na kwamba
waombaji wote wa manunuzi ya hati fungani wametaarifiwa na kwamba leo Agosti 2,
wanaorodhesha hati fungani zote, kabla ya wanunuzi kukabidhiwa vyeti mwezi
mmoja ujao.
Alifafanua
ya kwamba, mauzo hayo ya kiwango cha juu kuliko walivyotarajia, yanaiongezea
benki nguvu ya kiuchumi katika kufanikisha utoaji wa mikopo kwa wateja wao na
kwamba mchakato mzima umeshirikisha zaidi ya matawi 200 kote nchini.
“NMB
inatoa shukrani za dhati kwa taasisi zote zilizofanikisha uuzwaji wa toleo la
tatu la hati fungani ya NMB, ikiwemo CMSA, Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE),
Mshauri Kiongozi wa NMB, Stanbic Bank Tanzania Ltd na Dalali Mfadhili wa NMB,
Orbit Securities Company Ltd,” alisema Zaipuna.
Hati
fungani ni aina ya uwekezaji, ambao unamuwezesha mteja kuwekeza pesa katika
taasisi (hasa shirika la kibiashara au Serikali), kwa kuikopesha fedha kwa muda
maalum na kwa riba isiyobadilika. Riba ya hati fungani za NMB kwa mwaka ni
asilimia 10.
Mteja
anaponunua Hati Fungani ya NMB, anakuwa ameikopesha benki fedha zake, ambako
NMB inaahidi kurejesha fedha zake (msingi) katika kipindi maalum cha ukomavu.
Kuanzia muda uliowekeza hadi muda wa ukomavu ambao unakuwa miaka mitatu.
No comments:
Post a Comment