HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 03, 2019

DStv yazindua msimu mpya wa 'Soka Mwanzo Mwisho'

NA JANETH JOVIN

WAKATI pazia la Ligi za Ulaya likitarajiwa kufunguliwa wikiendi hii, ikiwemo Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), Kampuni ya DStv Tanzania imezindua msimu mpya wa soka wenye kauli mbiu  'Soka Mwanzo Mwisho' ambayo ni ya mwaka 2019/20.

Katika kuelekea katika huo uhondo wa kandanda, Wapenzi na mashabiki wa Ligi bora na pendwa Ulimwenguni  EPL pamoja na Ligi ya Italia na Hispania  wamehakikishiwa kushuhudia mitanange yote kupitia kingamuzi cha DStv ambacho kitarusha matangazo yote mubashara.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa msimu mpya wa Soka jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo, Ronald Shelukindo, anasema DStv inawahikikishia wateja wake wote kuendelea kushuhudia soka katika muonekana bora zaidi huku wakipata matangazo ya Ligi ya England EPL kwa Lugha adhimu ya Kiswahili.

"Kampeni yetu ya sasa tunasema ni ,Soka Mwanzo Mwisho, tunamaanisha kwani wateja wetu wa DStv, burudani ya soka haitawatindikia kamwe! Ni wapi unaweza kuona mechi zaidi ya 1000 za ligi kubwa duniani kama ligi ya England (EPL, Hispania (La Liga, Italia (Serie A, ligi ya Mabingwa Ulaya na nyingine nyingi, Bila shaka ni DStv pekee..ndiyo maana tunasema kwetu DStv ni Soka Mwanzo Mwisho!.

...Katika kuhakikisha kuwa burudani hiyo haimpiti mteja wa DStv, kwa kupitia app ya DStv Now wateja wataweza kuangalia popote walipo wakati wowote kwa kutumia vifaa kama simu, tablate na laptop. Pia mteja anayetumia DStv Now anaweza kuunganisha vifaa vine tofauti kwa kutumia akaunti moja bila malipo ya ziada..alisema Shelukindo," anasema Shelukindo.

Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na wadau wa soka nchini wakiwemo wasanii mbalimbali, wachezaji wastaafu na watangazaji wa ligi ya EPL kwa Kiswahili ambao ni Salma Jabir, Edo Kumwembe, Maulid Kitenge, Ibrahimu Masoud (Maestro, Abuubakari Lyongo na Oscar Oscar.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau hao wa soka walisema kitendo cha DStv kuonyesha ligi hizo kubwa mubashara ni fursa kubwa sio kwa washabiki tu wa soka bali pia hata kwa wanasoka wenyewe kwani ni ulingo muhimu wa kujifunza.

Sambamba na uzinduzi wa kampeni hiyo, DStv imetangaza ofa maalumu kwa wateja wapya wanaojiunga kuanzia Agosti mosi hadi Septemba 30 mwaka huu watajiunga na DStv kwa Sh, 99,000, na kupata kifurushi cha Family cha miezi miwili.

Pazia la msimu wa mpya wa soka litafunguliwa jumapili hii kwa mtanange wa ngao ya Jamii kati ya Liverpool dhidi ya Manchester City mchezo ambao utaonyeshwa mubashara kupitia DStv.

No comments:

Post a Comment

Pages