HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 09, 2019

WANASIMBA WAOMBWA KUISHANGILIA YANGA KESHO

NA HAJI MANARA

Imetuchukua miongo kadhaa kama nchi kupata fursa ya kuwakilishwa na klabu nne kwenye mashindano ya CAF, ni Simba wenye mchango mkubwa katika hili!!

Kama Taifa tunatakiwa tufanye vizuri zaidi kupitia wawakilishi wetu ili tuendelee kwa miaka ijayo kuwa na klabu nne katika mashindano ya CAF.

Najua ni ngumu kunielewa leo, lakini nawaomba Wanasimba wote kesho msiwazomee Yanga, msilipe kisasi na wekeni maslahi mapana ya nchi, sisi ni waungwana na uungwana ni vitendo!!

Kama hujiwezi usiende Taifa na ikibidi kwenda na huwezi kuwashangilia bora ukae kimya!!
Najua walitukera msimu uliopita lakini tuiangalie nchi kwanza na pia tujue wao, Azam na KMC pamoja na sisi ndio tuna nafasi ya kuendelea kupewa nafasi nne tena msimu ujao!!

Chondechonde watu wangu nieleweni katika hili, naiangalia Tanzania kama nchi, utani na kuzodoana kwetu utatugharimu sote kama kuwacheka tuwacheke baadae lakini kwa sasa 'interest' ya Tanzania iwe moja

No comments:

Post a Comment

Pages