Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua moja kati ya nyumba 10 za Askari
Polisi alizozifungua na kukabidhi funguo kwa Askari waliopangiwa kuishi
katika nyumba hizo mjini Shinyanga, Agosti 9, 2019. Kushoto ni Mkuu wa
Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellak na wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya
Shinyanga, Jasinta Mbaneko.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipanda mti baada ya kufungua nyumba
za makazi ya Askari Polisi mjini Shinyanga, Agosti 9, 2019. Kulia ni
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa
Shinyanga, Zaib Tellak.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Agosti 9, 2019 aliwakabidhi
funguo za nyumba Askari Polisi 10 baada ya kufungua nyumba za makazi
yao mjini Shinyanga. Pichani, Mheshimiwa Majaliwa akimkabidhi, Koplo
Tegemea Masatu ufungua wa nyumba aliyopangiwa kuishi. Katikati ni
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Shinyanga, ACP Richard Abwao.
No comments:
Post a Comment