HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 10, 2019

Nchi za SADC zakaribishwa MNH, MOI, JKCI

NA SULEIMAN MSUYA

NCHI wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kutumia Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Taasasi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kupata tiba bora na za kisasa.

Ombi hilo limetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati akizungumzia na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam alipotembekea mabanda ya taasisi mbalimbali yanayoshiriki Maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya SADC.

Waziri Mwalimu alisema hospitali ya MNH, JKCI na MOI zimeboreshwa kwa kupata vifaa vya kisasa hivyo  ni fursa pekee kwa nchi za SADC kutumia na kuachana na utaratibu wa kupeleka wagonjwa nje.

Alisema kwa sasa kuna vyumba vya upasuaji zaidi 40 kutoka nane kabla ya mwaka 2015 hali ambayo inarahisisha huduma hiyo.

"Tumewekeza kwa kiwango kikubwa kwa sasa tunatoa huduma ya upandikizaji wa figo, vifaa vya kusikia Watoto na huduma nyingine za kibingwa hapa nchini hivyo kupunguza gharama za kwenda Afrika Kusini na India, tunazikaribisha nchi za SADC zilete wagonjwa wao," alisema.

Alisema hospitali hizo zimejipanga kutoa huduma za kimataifa kwa washiriki wa mkutano wa SADC ikiwa ni pamoja na kueleza tiba zinazotolewa nchini.

Alisema Hospitali ya Muhimbili kwa mwezi inapokea wagonjwa 24 kutoka nchi za SADC ambazo ni Comoro, Malawi na DRC Congo.

"Kwa mwaka tunapokea wagonjwa 284 ni matarajio yetu baada ya mkutano huo idadi itaongezeka kwani tumejipanga kutoa huduma nzuri," alisema.

Mwalimu alisema jitihada za Serikali ni kuongeza wataalam wengi zaidi ili kuweza kukidhi hitaji la nchi  na nchi za SADC.

Alisema mwaka huu wamepata ufadhili wa kusomesha zaidi ya madaktari bingwa 25 hadi 50 ili waweze kusomea utaalam mbalimbali.

Aidha, Waziri Ummy alisema Tanzania imepata zabuni ya kusambaza dawa katika nchi za SADC, kupitia Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na imeonesha uwezo mkubwa.

Alisema mfumo huo wa ununuzi wa dawa kwa pamoja umeonesha unafuu kwa zaidi ya asilimia 40.

No comments:

Post a Comment

Pages