MBUNGE wa Singida Kaskazini Justine Monko amempongeza Rais John Magufuli kwa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya maendeleo ya nchi zilizopo Kusini mwa Bara la Afrika (SADC) katika mkutano wa 39 wa Jumuiya hiyo uliomalizika Jumapili Jijini Dar es Salaa.
Akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari, Monko alisema hatua ya Rais Magufuli kuteuliwa katika nafasi hiyo ni faraja kwa watanzania wote wakiwemo wananchi wa Jimbo la Singida Kaskazini ambao siku zote wamekuwa wakimuunga mkono kwa juhudi zake za kulileta Taifa maendeleo.
Alisema yeye pamoja na wananchi wa Singida Kaskazini wana imani kubwa na Mwenyekiti huyo mpya wa SADC katika wadhifa wake huo mpya kutokana na kuonyesha mafanikio mazuri ya uongozi wake katika Taifa tangu alipochaguliwa kuwa Rais wa taifa hili katika uchaguzi wa Mwaka 2015.
“Tunaamini ataitendea haki SADC kama ambavyo amekuwa akifanya katika Taifa hili, kwani katika kipindi ambacho amekuwepo madarakani ameweza kufanya mambo makubwa ya kimaendeleo na ujenzi wa uchumi kitu ambacho watu wengi hawakudhani kama kingafanyika, imani hiyo aliyotupa ndiyo tunayoamini kuwa ataiendeleza SADC” alisema Monko.
Aidha alisema pamoja na kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC pia mkutano huo wa wakuu wa nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo ulifana chini ya Uenyeji wake huku hotuba yake ikigusia maeneo muhimu kwa ajili ya Maendeleo ya Jumuiya hiyo na Wananchi wake, jambo alilodai kuwa litazidi kuhimarisha Umoja na mshikamano wa Nchi hizo kama alivyokuwa ameligusia katika hotuba yake alipokuwa akifunga mkutano huo.
Monko alisema kauli ya Rais Magufuli kusema kuwa Tanzania ipo tayari kutoa ushirikiano unaohitajika kwa wanachama wa SADC ili kuharakisha jitihada za kuleta maendeleo fungamani, linaonyesha ni kwa namna gani Kiongozi huyo ana kiu ya kuziona nchi zote zilizomo ndani ya SADC zinapiga hatua zaidi za kimaendeleo kama alivyo na kiu hiyo kwa Tanzania .
Alisema kimsingi mambo mengi ambayo Rais Magufuli amegusia katika hotuba yake hiyo yana akisi yale anayoendelea kuyafanya hapa nchini ambayo kwa kiasi kikubwa matokeo yake yanaonekana kwa kadri siku zinavyozidi kwenda huku akitoa rai kwa Mataifa Wanachama wa SADC kuyatekeleza ili malengo yaliyokusudiwa yaweze kufikiwa.
Aidha alisema hatua ya Rais Magufuli kuzitaka nchi wanachama wa Jumuiya hiyo kuweka mkazo katika usimamizi wa rasimali zake una maana kubwa katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi miongoni mwa nchi wanachama ambapo pato lake la ukuaji wa uchumi kwa Taifa ni wastani wa asilimia 22 katika kipindi cha Mwaka 2018.
Kuhusu lugha ya Kiswahili kuchaguliwa kuwa miongoni lugha ya nne za kimataifa kutumika katika mikutano ya SADC, Mbunge huyo alisema kunaleta fahari kwa Tanzania kwa kuwa itazidi kulitangaza Taifa na kuzidi kuliletea heshima katika Mataifa mbalimbali huku tayari lugha hiyo ikitajwa kuzungumzwa katika mataifa 10 Duniani.
Amesema wananchi hao wa Singida Kaskazini wamaamini pia katika falsafa yake ya Hapa Kazi tu jambo linalowafanya wajitume kila siku ili kujiletea maendeleo

No comments:
Post a Comment