Na Mwandishi Wetu, Morogoro
MWENYEKITI
wa Serikali ya Mtaa wa Mbwamaji uliopo Gezaulole Kata ya Somangila Wilayani
Kigamboni, Dar es Salaam, Yohana Maziku ametoa
salamu za pole kufuatia ajali ya moto Mkoani hapa iliyosababisha vifo vya watu
zaidi ya 60, majeruhi mbalimbali.
Maziku aliungana
na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Waziri mkuu Kasim Majaliwa waliofika kutoa pole pamoja na shughuli za
mazishi akiwakilisha Wananchi wa Gezaulole Mbwamaji, amebainisha kuwa kuwepo na
ukaguzi wa mara kwa mara kwa magari yote yanayobeba vimiminika ikiwemo mafuta,
gesi na viambata sumu kwani kwa kufanya hivyo vitasaidia kupunguza ajali na
matukio ya vifo vya mara kwa mara.
Pia
amezishauri mamlaka zinazoshughulikia kwa kila mmoja kufanya kazi yake kwani
katika ili uzembe umechangia kwa asilimia kubwa.
“Mamlaka
zifanye kazi yake. Magari haya hayakaguliwi ipasavyo madereva nao wanatumia
mwanya huo na baadae tunaendelea kushuhudia majanga makubwa kama haya.”alisema
Maziku.
Akituma
salama zake kutoka kwa wananchi wa Mbwamaji Gezaulole, alisema :“Nasikitika sana kwa maafa yaliyotokea
kwani tumepoteza watanzania wengi tena nguvu kazi ya taifa letu. hii inauma
sana kuna asilimia kubwa sana kuwa ilipotokea ajali ya kuanguka kwa lori la
mafuta kunauzembe ulifanywa juu ya viongozi wa ngazi za chini yaani ngazi ya
Mtaa, Kata na jeshi la Polisi kwani ninaimani kuwa wangesimamia kuwazuia
wananchi hao kuiba mafuta au kusogelea kwenye tukio ninaamini tusinge kuwa na
idadi kubwa ya marehemu na majeruhi kama
hii sasa” alieleza Maziku.
Aidha,
Maziku aliongeza kuwa: Kupitia tukio hilo liwe fundisho kwa Watanzania wote huku pia akiwataka viongozi
kwa ujumla kila mmoja atimize wajibu wake huku akiishukuru Serikali kupitia
Rais Magufuli kwa kuonyesha ushirikiano mkubwa kwa familia za wafiwa na familia
za majeruhi.
Katika tukio
hilo lililotokea asubuhi ya Agosti 10, baada ya lori la mafuta kupinduka eneo
la Msamvu, wananchi mbalimbali walijitokeza kuchota mafuta na baadae liliweza
kulipuka na kusababisha majeruhi na vifo kwa wananchi hao.
No comments:
Post a Comment