Mwenyekiti wa umoja
wa Wakuu wa Shule za Sekondari (TAHOSA) mkoani Tabora Penini Shani
akitoa salamu za umoja huo wakati wa Mkutano wa TAHOSA Mkoa wa Tabora
hivi karibuni.
NA TIGANYA VINCENT
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora
imesema haitasita kuwachukulia hatua Wakuu wa Shule za Sekondari na Msingi ambao
watakuwa na wanafunzi wengi waliopata Daraja la nne na Sifuri.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Katibu
Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu wakati wa mkutano wa
umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari (TAHOSA) mkoani Tabora.
Alisema Shule
zinazozalisha sifuri na Daraja la nne (division four) kwa wingi ndizo
zinasababisha Mkoa wa Tabora kutoshika nafasi ya kwanza katika matokeo
mbalimbali ya kumaliza elimu ya msingi na Sekondari.
“Hatutasita kumchukulia
hatua wale wanaotuvutavuta shati tuzifanye vizuri na hivyo kuwa na watoto
waliopata sifuri na Daraja la nne kwa wingi…ni vema tufanya kazi kwa bidi na tujitadi
kuondoa sifuri na kupunguza Daraja la nne mkoani kwetu” alisisitiza.
Alisema kuwa uwezo wa
kuondoa sifuri na kupunguza Daraja la Nne upo kwa kuwa Shule ambazo wanafunzi
wanafanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho wanafundishwa na walimu sawa na
wale walio Tabora na wamepata Mafunzo ya ualimu katika vyuo vil vile ambavyo
walimu wa Tabora walipitia.
Makungu alisema walimu
wakafanyakazi kwa bidii ili kuongeza idadi ya Shule za Msingi na sekondari nyingi
zinazofanya vizuri ikiwemo kuingia katika kumi bora kitaifa na kuufanya Mkoa wa
Tabora kutoka namba nane kuwa kwenye tatu bora Kitaifa.
Mwenyekiti wa umoja wa Wakuu
wa Shule za Sekondari (TAHOSA) mkoani Tabora Penina Shani aliupongeza Uongozi
wa Mkoa wa Tabora kwa kampeni yao inayoendelea ya kuondoa Daraja la sifuri na
la nne.
Alisema hatua hiyo
imesaidia baadhi ya Shule kushika nafasi za juu kitaifa ikiwemo Shule ya
Wavulana ya Tabora ambayo imekuwa ya tano kitaifa katima matokeo ya kidato cha
Sita.
Shani alisema kupitia
TAHOSA Mkoani wameendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha elimu na
kuongeza ufaulu kwa ngazi zote.
No comments:
Post a Comment