HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 12, 2019

Mwenyekiti Serikali ya Mtaa Mbwamaji atoa tahadhari majanga ya moto nchini

Na Mwandishi Wetu, Morogoro
MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa wa Mbwamaji uliopo Gezaulole Kata ya Somangila Wilayani Kigamboni, Dar es Salaam,  Yohana Maziku ametoa salamu za pole kufuatia ajali ya moto Mkoani hapa iliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 60, majeruhi mbalimbali.
Maziku aliungana na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Waziri mkuu Kasim Majaliwa  waliofika kutoa pole pamoja na shughuli za mazishi akiwakilisha Wananchi wa Gezaulole Mbwamaji, amebainisha kuwa kuwepo na ukaguzi wa mara kwa mara kwa magari yote yanayobeba vimiminika ikiwemo mafuta, gesi na viambata sumu kwani kwa kufanya hivyo vitasaidia kupunguza ajali na matukio ya vifo vya mara kwa mara.
Pia amezishauri mamlaka zinazoshughulikia kwa kila mmoja kufanya kazi yake kwani katika ili uzembe umechangia kwa asilimia kubwa.
“Mamlaka zifanye kazi yake. Magari haya hayakaguliwi ipasavyo madereva nao wanatumia mwanya huo na baadae tunaendelea kushuhudia majanga makubwa kama haya.”alisema Maziku.
Akituma salama zake kutoka kwa wananchi wa Mbwamaji Gezaulole,  alisema :“Nasikitika sana kwa maafa yaliyotokea kwani tumepoteza watanzania wengi tena nguvu kazi ya taifa letu. hii inauma sana kuna asilimia kubwa sana kuwa ilipotokea ajali ya kuanguka kwa lori la mafuta kunauzembe ulifanywa juu ya viongozi wa ngazi za chini yaani ngazi ya Mtaa, Kata na jeshi la Polisi kwani ninaimani kuwa wangesimamia kuwazuia wananchi hao kuiba mafuta au kusogelea kwenye tukio ninaamini tusinge kuwa na idadi kubwa ya marehemu  na majeruhi kama hii sasa” alieleza Maziku.
Aidha, Maziku aliongeza kuwa: Kupitia tukio hilo liwe fundisho  kwa Watanzania wote huku pia akiwataka viongozi kwa ujumla kila mmoja atimize wajibu wake huku akiishukuru Serikali kupitia Rais Magufuli kwa kuonyesha ushirikiano mkubwa kwa familia za wafiwa na familia za majeruhi.
Katika tukio hilo lililotokea asubuhi ya Agosti 10, baada ya lori la mafuta kupinduka eneo la Msamvu, wananchi mbalimbali walijitokeza kuchota mafuta na baadae liliweza kulipuka na kusababisha majeruhi na vifo kwa wananchi hao.

No comments:

Post a Comment

Pages