HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 23, 2019

Wajane Misenyi wagaragara kwa serikali

NA LYDIA LUGAKILA, KAGERA

BAADHI  ya wanawake wajane wilayani Misenyi mkoani Kagera waimeomba serikali kuwapa kipaumbele pale zinapotolewa fursa mbalimbali zikiwemo za mikopo na mgawo wa fedha zinazotolewa kwa ajili ya kunusuru kaya maskini ili waondokane na vikwazo wavipatavyo baada ya kuondokewa na waume zao.


Hayo yamebainishwa wilayani Misenyi mkoani Kagera wakati baadhi ya wanawake hao wakizungumzia changamoto na vikwazo vinavyowakumba mara baada ya waume zao kufariki dunia.


Elieth Elieza ni mama wa watoto sita ambao wanasoma shule na walioacha shule kabisa kutokana na vikwazo  mbalimbali ikiwemo uwezo wa kifedha na kielimu vinavyowafanya wanawake hao kutosonga mbele.


Elieza alisema kuwa kabla ya mume wake kufariki hali ilikuwa nzuri lakini kwa sasa vikwazo ni vingi ambapo amedai kuwa kuna haja  kwa serikali na wadau wengine kuwasaidia kwa namna moja hama nyingine kwa kuwapa vipaumbele ili kuwasaidia kuondokana na vikwazo hivyo pale wanapoondokewa na waume zao.


 ”Kwa niaba ya wenzangu naiomba serikali itusaidie kutupatia kipaumbele katika fursa mbalimbali na kututatulia vikwazo vilivyopo,” alisema Elieza.


 Akitaja vikwazo vingine vinavyowakwaza alisema wajane wamekuwa wakikosa stahiki zao ikiwemo mirathi, mila na desturi zinazowakandamiza wanawake hao wajane huku wakitaja ndugu wa mume kuwa kikwazo pale mume anapoondoka  kwani hudhulumiwa mali.


Aliiomba  serikali iwasikilize hasa pale mashtaka yao yanapofikishwa mahakamani ili yapate suluhisho ili kunusuru mali za watoto wanaoachwa na wazazi wao.
Aidha Elieza alitaja changamoto kubwa aliyokumbana nayo tangu mwaka 2014 pale ndugu wa mume walipotaka arithiwe na mmoja wa ndugu wa mume wake.

No comments:

Post a Comment

Pages