Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola aliyekaa kwenye Pikipiki
akifurahia jambo na Mbunge wa Kilolo (CCM), Venance Mwamoto mara baada
ya Munge huyo kukabidhi msaada wa Pikipiki mbili ili zitumike na Jeshi
la Polisi Mkoa wa Iringa. Katikati ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa,
ACP Juma Bwire. (Picha na Datus Mahendeka, Jeshi la Polisi).
Na Datus Mahendeka, Jeshi la Polisi
WAZIRI wa
Mambo ya Ndani ya Polisi, Kangi Lugola amepokea msaada wa Pikipiki amanbazo
zitatumika kwa ajili ya doria ili kupunguza uhalifu Mkoa wa Iringa.
Aidha, amelitaka
Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kutotumia Pikipiki hizo kwa ajili ya kazi za
kihalifu ikiwemo kusingikiza mirungi na badala yake zitumike kwa kazi
iliyokusudiwa.
Lugola
alitoa kauli hiyo jana, wakati akipokea msaada wa Pikipiki mbili zenye thamani
ya Tsh 2.8 zilizotolewa na Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto kwa ajili ya kituo
cha Ikokoto Iringa.
“Tumepokea Pikipiki
hizi…wazitunze ili zidumu.. zitumike kwa
ajili ya kufanya doria kwenye maeneo korofi hususani maeneo ya mlima
Kitonga”alisisitiza.
Hata hivyo
alitoa wito kwa wananchi na wadau werevu kuendelea kulisaidia jeshi la polisi
kamwe wasichoke kutoa misaada kwa Jeshi la polisi.
No comments:
Post a Comment