HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 27, 2019

BENKI YA CRDB YAZINDUA KAMPENI YA 'ULIPO TUPO'

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulamajid Nsekela, akisalimiana na baadhi ya wateja wa benki hiyo waliofika katika uzinduzi wa Kampeni ya 'Ulipo Tupo'
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulamajid Nsekela, akisalimiana na baadhi ya maofisa wa benki hiyo.
 Mkurugenzi wa Wateja wa Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya 'Ulipo-Tupo' jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB, Dk. Joseph Witts, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya 'Ulipo Tupo'
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto), akifuatilia hotuba ya Ofisa Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB, Dk. Joseph Witts.
  Ofisa Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB, Dk. Joseph Witts, akiongezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela (kushoto) wakati uzinduzi wa Kampeni ya 'Ulipo Tupo'
 Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya CRDB, Joseline Kamuhanda, akizungumza katika hafla hiyo.
Wakurugenzi wa Beni ya CRDB.
Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya CRDB, Joseline Kamuhanda, akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, kuzungumza katika hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, kutoa hotuba yake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, kutoa hotuba yake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, kutoa hotuba yake.











Na Mwandishi Wetu

Benki ya CRDB imezindua Kampeni ya Ulipo Tupo ambayo ina lengo la kuendelea kuwakumbusha wateja wake na watanzania kwa ujumla juu ya huduma zitolewazo na Benki ya CRDB ambazo zinamlenga mtanzania mmoja mmoja. 

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni huo, Ofisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts, alisema “kwa muda mrefu sasa, Benki ya CRDB imekuwa ikitumia kauli mbiu yake ya Ulipo Tupo ikibeba ahadi kwa wateja wetu kuwa sisi kama Benki Tupo na tunaendelea kuwepo popote pale wateja wetu walipo ili kufanikisha malengo tuliojiwekea" leo hii tunazidua rasmi kampeni ya 'Ulipo-Tupo'

Benki ya CRDB inaendelea kuwakumbusha na kuwasisitiza watanzania kuhusu njia mbadala za kujiwekea akiba ambazo zinatolewa na Benki ya CRDB. Alisema Dkt. Joseph Witts “Benki ina bidhaa mbalimbali ambazo zitaweza kusaidia wateja na watanzania kwa ujumla kutimiza malengo na mahitaji yao kwa kujiwekea akiba kwa ajili ya baadae. Bidhaa hizi ni kama;  

“Benki imejikita katika kutoa mikopo mbali mbali kwa vikndi mbali mbali kwa riba nafuu na kwa haraka zaidi kwa kupunguza masharti yake ili kumuwezesha kima mtanzania kuweza kukopa na kufikia malengo yake aliyojiwekea." alisema Dkt. Witts.

Benki imejikita kutanua mtandao wake ili kuwafikia watanzania wote na kutoa huduma bora za kibenki kupitia
Huduma za kadi za kimataifa (Visa cards, Master cards, China union pay) Huduma za mtandao (internet banking) 

Ofisa Biashara Mkuu wa Benki. Dkt. Joseph Witts, alisisitiza tena kwa kusema “ Lengo la Benki ya CRDB ni kuhakikisha tunakuwa sehemu ya mafanikio ya maisha ya wateja wetu na watanzania kwa ujumla. 

Tunaendelea kukuza mtandao wetu na kueneza nchi nzima ili kuwafikia hata wale ambao bado hawajaflkiwa na huduma za kibenki na pia tuna mikakati mbadala ya kuboresha huduma zetu kupitia mifumo ya kidijitali, tukiishi kwa kauli yetu hai ya “Uli-Tupo” 

No comments:

Post a Comment

Pages