Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera Mhe. Hashim Ngeze akizungumza na waandishi wa habari.
Na Lydia Lugakila Kagera
Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera
imefanikiwa kwa asilimia 98 kukamilisha maandalizi ya Mtihani kwa wahitimu wa
darasa la saba 2019 unaotarajiwa kufanyika
Septemba 11-12 Mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa Septemba 7,
2019, na Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera Mhe. Hashim Ngeze
wakati akizungumza na vyombo vya habari
katika ofisi za halmashauri hiyo zilizopo mkoani hapa.
Ngeze amesema hadi sasa Mitihani hiyo tayari imeishawasili
wilayani humo na zoezi la kuingawa
kwenda shule za msingi ili kila shule
iweze kuipata mitihani yake ambapo pia kiasi cha fedha kwa ajili ya kusimamia mitihani hiyo tayari kimeletwa na bajeti imeishakuwa tayari maandalizi
yako vizuri na kutaja maandalizi hayo kufikia asilimia 98.
Mhe. Ngeze amesema Halmashauri hiyo
ina shule 141 za kiserikali na 8 za
binafsi huku akitaja jumla ya wanafunzi ambao
wanatarajia kufanya mitihani wilayani humo kuwa wasichana ni 3511 na wavulana
ni 3351.
amesema anatarajia matokeo mazuri sana kwa kuwa hivi karibuni
serikali imetoa pikipiki kwa waratibu wa elimu kata kwa hiyo ufuatiliaji
wa shule ya msingi unaenda vizuri ambapo
amedai kuwa hata kwa mitihani ya ndani wa shule ya msingi kujipima wanafunzi
walifanya vizuri kutokana na usimamizi mzuri.
‘’Wito wangu kwa wazazi na walezi wa
watoto wanaotarajia kufanya Mtihani huo
ni kuwa karibu na watoto kuwaliwaza,ili wasiwe na mawazo wakiwa ndani ya
Mtihani kwa sababu kushindwa kwa mtihani kunaanzia na maandalizi ya mtoto kutoka
nyumbani anapoingia ndani ya chumba cha
Mtihani ana mawazo jambo hilo linalosababisha kushindwa kufuata maelekezo ya mtihani, kwa hiyo wazazi kwa kipindi hiki
toeni uhuru kwa watoto wenu na mkawape ushauri wa jinsi ya kutulia na kufanya
mitihani yao vizuri,,’’amesema.
Amesema kuwa kumekuwepo na tabia ya
baadhi ya wazazi wanaowashinikiza watoto wao wasifanye vizuri mitihani yao ili
kushinda kuingia kidato cha kwanza kwa sababu ya umbali mrefu wa kufuata shule
huku akitolea mfano shule ya msingi Kasharu na Rukoma kuwa hilo limekuwa
likifanyika.
Ameongeza kuwa alitembele shule ya
msingi Kamukore kati ya wanafunzi 19 wanafunzi 7 walikiri kwamba wazazi wao
wameishawaambia wasifanye vizuri mtihani wao wa darasa la saba kwa sababu ya
ukosefu wa shule ya sekondari amewataka
wazazi kutolipa kipaumbele suala hilo ili watoto wao wapate elimu sitahiki na
kutimiza ndoto zao.
Amesema zaidi ya shilingi milioni 600 zimepokelewa kutoka serikali ili kuwezesha
elimu bila malipo na kumshukuru Rais Dokt.
John Magufuli kwa kuanzisha utaratibu wa elimu bila malipo kwa sababu
inaondolea wazazi mzigo wa kulalamika.
No comments:
Post a Comment