HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 06, 2019

CHUO KIKUU MZUMBE CHATOA MAFUNZO YA UELEDI

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Prof. Honest Ngowi, akimkadhi cheti, Gloria Mabada, mmoja wa washiriki wa mafunzo ya kupata ueledi wa utekelezaji wa miradi iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo, mafunzo hayo yaliandaliwa na chuo hicho. Kulia ni Mwezeshaji wa mafunzo hayo, Dk. Muhajir Kachwamba. (Picha na Francis Dande).
Mwezeshaji wa mafunzo Dk. Muhajir Kachwamba, akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo.
Mwezeshaji wa mafunzo Dk. Muhajir Kachwamba, akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo.
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Prof. Honest Ngowi, akifunga mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki.
Baadhi ya washiriki.

Meza Kuu.

Mhadhiri Msaidizi kutoka Chuo cha Mipango Dodoma, Kiula P. Kiula, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wenzake.
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Prof. Honest Ngowi, akibadilishana mawazo na Dk. Muhajir Kachwamba.

Mshiriki kutoka Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar, Hawa Khamis Juma.
Picha ya pamoja.

Na Mwandishi Wetu

CHUO Kikuu Mzumbe kimetoa mafunzo ya ueledi wa miradi mbalimbali kwa watendaji wa baadhi ya taasisi binafsi na serikali.

Kwa mujibu wa mwezeshaji wa mafunzo hayo, Dk. Muhajir Kachwamba malengo ya mafunzo hayo ni kupatia ueledi wa kuandika miradi na masuala ya bajeti kwa wakati.

“Tumetoa mafunzo ya ueledi kwa miradi mbalimbali kwa muda wa wiki nzima, lengo likiwa ni kujifunza namna bora ya kuandaa miradi kuanzia mipango inavyopangwa na bajeti kwa wakati stahili,” alisema Dk. Kachwamba.

Dk. Kachwamba aliweka bayana taasisi zilizopata mafunzo hayo ni pamoja na Chuo cha Mipango, Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu, miradi mbalimbali kama waratibu wa miradi mbalimbali,

Wamemalizia mafunzo hayo kwa jambo muhimu ambalo ni utumiaji wa teknolojia za kisasa kama Kompyuta ambayo inarahisisha utoaji wa ripoti kwa maendeleo ya miradi kadri miradi inavyokuwa inatekelezwa.

No comments:

Post a Comment

Pages