HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 06, 2019

RAIS DKT MAGUFULI NA RAIS WA UGANDA MHE MUSEVENI WAHUTUBIA KONGAMANO LA BIASHARA, WAZINDUA JENGO LA TAASISI YA MWALIMU NYERERE

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimwonesha  Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni baadhi ya picha na maelezo ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa walipowasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini kwa ajili ya Kongamano la Wafanyabishara wa Tanzania na Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiomba wahudhuriaji kusimama kwa dakika tatu za heshima ya kumkumbuka aliyekuwa Rais wa Zimbabwe Marehemu Robert Mugabe aliyefariki leo huko Singapore akiwa katika matibabu. Hii ilikuwa ni kabla ya kuanza kuhutubia Kongamano la Wafanyabishara wa Tanzania na Uganda lililohudhuriwa pia na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri Museveni wakipata maelezo kutoka kwa  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB,  Abdulmajid Nsekela, walipotembelea vibanda vya maonesho  wakati wa Kongamano la Wafanyabishara wa Tanzania na Uganda katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akipeana mikono na mgeni wake  Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, baada ya kufungua rasmi jengo la Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli na mgeni wake  Rais wa Uganda, Yoweri Museveni wakisaidiwa na viongozi  wengine wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli na mgeni wake  Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni wakitembezwa na Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere Julius Nyerere, Joseph Butiku ndani ya jengo walilolifungua kwa pamoja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli na mgeni wake  Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wanafamilia wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage nyerere wakati wa sherehe za ufunguzi  rasmi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere. PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment

Pages