HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 18, 2019

HALMASHAURI ZATAKIWA KUACHA URASIMU UTOAJI MIKOPO KAGERA

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Halima Bulembo, akizungumza na wananchi.

Lydia Lugakila, Kagera

Vijana mkoani Kagera wametakiwa kuzitolea taarifa halmshauri zote za mkoa huo mbazo zinakwama kutoa mikopo kwa vijana na akina mama.

Kauli hiyo imetolewa Septemba 17, 2019 na Mbunge wa Vijana Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Kagera, Halima Bulembo, wakati akizunguza na wananchi katika uzinduzi wa Misenyi ya Kijani uliofanyika wilayani humo. 
 
Mbunge huyo amewataka vijana  kuzitolea taarifa halmashauri ambazo hazitoi mikopo kwa kwani kwa kufanya hivyo ni kurudisha maendeleo ya kundi hilo  nyuma  na taifa kwa ujumla.
 
Bulembo ametoa kauli hiyo baada ya kugundua Suala la utoaji  mikopo kwa vijana na akina mama kuonekana kusuasua ‘’Mara utaambiwa kikundi hiki hakijitoshelezi, mara umezidi umri, figisu figisu za nini? Nawaambia vijana wenzangu jiamini  mikopo ni haki yenu hamfanyiwi hisani mnatakiwa kukopeshwa,’’amesema Mbunge huyo amesema vijana ni taifa la leo ambapo biblia na Quran zinasema kesho kuna kifo.

Aliongeza kuwa mikopo itoke ili vijana wajiajiri ili kuliendeleza taifa lenye maendeleo na kutoa wito kwa vijana katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa  kujitokeza kugombea nafasi mbali mbali za uchaguzi na Kuacha kulalamika Badala yake wafanye shughuli za maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Pages