HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 24, 2019

MABINGWA NGUMI KUPONGEZWA NA MASHABIKI OKTOBA 4

Mabondia wa mgumi za kulipwa nchini walioibuka na ushindi wanatarajia kushiriki katika sherehe za kupongezwa na mashabiki wao Oktoba Nne Club 361Mwenge Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi Mratibu mkuu wa Pambano la kuwapongeza mabondia hao Selemani Semunyu alisema mipango imekamilika ikiwemo mabondia watakaocheza ingawa maombi ni mengi ya mabondia wengi kutaka kushiriki kuonyesha furaha yao na kuwaunga mkono mabondia hao.

Aliwataja miongoni mwa mabingwa  hao ni  Abdalah Pazi ,Tonny Rashidi ,Bruno Vifua Viwili na  Nassib Ramadhani kwa pamoja na bondia yeyote binhwa na wameletea taifa heshma kubwa  wadau na mashabiki hakuna budi kuwapongeza.

" Serikali na Wabunge wamewapongeza lakini wadau na mashabiki sasa huu ndio wasaa wa kuwapongeza hata kama kuna zawadi ya kuwapa hii ndio sehemu moja lakini sie tunawapongeza kwa pambano" Alisema Semunyu.

Aliongeza kuwa pambano hili pia litatumika kupata mabondia watakaowania mikanda mwezi Desemba ambapo litafanyika pambano funga mwaka.


" Watakaofanya vizuri katika pambano hili wataweza kupata nafasi katika pambano la mwezi wa 12 ambapo historia ya Ngumi nchini kwa  kipindi cha hivi karibuni utawekwa " Alisema Semunyu.

Pia amewashukuru kamisheni ya ngumi za kulipwa kutoa kibali wadhamini Smart Gin na kuomba wadhamini wengine kujitokezo kwa wingi ili kufanikisha kurejesha hadhi ya mchezo wa ngumi nchini.

Kwa upande wake mratibu wa kiufundi wa mapambano hayo Yassin Abdalah  Ustaadh aliwataja mabondia watakaosindikiza sherehe hiyo kuwa ni issa nampechehe  (Dsm) vs alli hamisi  (morogoro )

Ibrahim Makubi (Dsm)vs abdallah kingolwira  (Morogoro) Maganga kulwa (mbagala) vs Said Sudi (M'nyamala) Hashimu msungo vs Epson John Lewis Salumu Omari vs Ramadhani Chicho.

Aliongeza kuwa mapambano yanaweza kuongezeka kutokana na  mabondia wengine kitafuta nafasi ya kutaka kishiriki Desemba lakini wengine nao wanatala kushiriki kuonuesha furaha ya ushindi huo

" Mapambano ya surprize kibao  mabingwa watakuwepo  na wasanii wa kutumbuiza njoo tuwapongeze mabondia wetu walioshinda mikanda tule tunywe tupige nao picha," alisema Ustaadh.

No comments:

Post a Comment

Pages