Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili nchini Zimbabwe kuhudhuri mazishi ya kitaifa ya aliyekuwa Rais wa Zimbabwe marehemu Robert Mugabe aliyefariki wakati akipatiwa matibabu nchini Singapore wiki iliyopita.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisaini kitabu cha maombolezo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Rais Mstaafu wa Zambia Mhe. Keneth Kaunda na Rais Mstaafu wa Nigeria Mhe. Olubagan Obasanjo wakiteremka kwenye Jukwaa baada ya kutoa Heshima za Mwisho mbele ya Jeneza lenye Mwili wa Rais wa Zamani na Muasisi wa Taifa la Zimbabwe Marehemu Mzee Robert Gabriel Mugabe katika Uwanja wa Taifa wa Michezo jijini Harare Zimbabwe. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Hafla hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais Kenya Mhe. Uhuru Kenyata walipokutana wakati wa Hafla ya kutowa Heshima za Mwisho mbele ya Jeneza lenye Mwili wa Rais wa Zamani na Muasisi wa Taifa la Zimbabwe Marehemu Mzee Robert Gabriel Mugabe katika Uwanja wa Taifa wa Michezo jijini Harare Zimbabwe. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Hafla hiyo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).


No comments:
Post a Comment