Mbunge wa Vijana Mkoa wa Kagera, Halima Bulembo, akimkabidhi Printa 10 na Kompyuta 10
kwa ajili ya Makatibu wa Wilaya 8 wilayani Muleba.
Katibu wa CCM Mkoa wa Kagera, Raheli Ndegereki (kulia), akipokea msaada kutoka kwa mbunge wa vijana, Halima Bulembo.
Na Lydia Lugakila, Bukoba
Mbunge wa Vijana
CCM Mkoa wa Kagera, Halima Bulembo amekabidhi Printer 10 na Kompyuta 10
kwa makatibu wa wilaya 8 wa mkoa huo ili kuunga mkono shughuli za chama hicho kufanyika bila vikwaz0.
Mhe. Bulembo amekabidhi vifaa hivyo
Septemba 20,2019 katika ofisi za chama hicho zilizopo katika manispaa ya Bukoba
mkoani Kagera ikiwa ni kuunga mkono shughuli za chama hicho kusonga mbele na
kuwesha wanachama wa chama hicho kutenda kufanya kazi za chama hicho bila kuwa
na changamoto.
Akiwa Manispaa ya Bukoba mbunge huyo
amemkabidhi printer moja na computer
moja ofisi ya mkoa huku akihaidi kuendelea kutoa ushirikiana kwa viongozi hao
pamoja na kuwaunga mkono vijana.
Katibu wa CCM Mkoa, Raheli Ndegereki, ameahidi kutumia vifaa hivyo vizuri kwa shughuli za chama
huku akimpongeza mbunge huyo.
Hata hivyo viongozi hao akiwemo katibu
wa mkoa wa Kagera vijana Salum Suleiman Tate na Katibu wa wilaya vijana
wilayani Muleba Athuman Sagara wamefurahishwa na suala hilo na kuwataka
viongozi wengine kuwa mfano bra.
No comments:
Post a Comment