Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu
Kijaji (Mb).
Na
Peter Haule na Farida Ramadhani, WFM, Dodoma
Serikali
kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina inaendelea na taratibu za kuwalipa waliokuwa
wafanyakazi wa Kiwanda cha Nguo cha Musoma (Musoma Textile Mills Limited Mutex)
kwa mwaka wa fedha 2019/20, baada ya uhakiki kukamilika mwezi Juni, 2019.
Hayo yameelezwa
Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu
Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Viti Maalum,
Mhe. Joyce Sokombi, aliyetaka kujua utofauti wa malipo kwa waliokuwa
wafanyakazi wa Kiwanda cha Mutex baada ya kufungwa mwaka 1984.
Dkt.
Kijaji alisema kuwa, Serikali inafuatilia kwa karibu malalamiko yote
yanayohusu tofauti ya kiwango cha malipo yaliyofanyika hivi karibuni
ikilinganishwa na kiwango kilichoidhinishwa kwenye kikao cha pamoja kati ya
Mfilisi wa Kiwanda hicho, wadau na Serikali ili kuona kama yana ukweli wowote.
“Baada
ya Serikali kupokea maombi ya malipo kutoka kwa wafanyakazi hao mwaka 2018,
Ofisi ya Msajili wa Hazina ilifanya uhakiki wa wafanyakazi hao ili kujiridhisha
na hatimaye kufanya malipo”, alieleza Dkt. Kijaji.
Alisema
kuwa awali jumla ya wafanyakazi 219 walijitokeza na wasimamizi wa mirathi 14 na
hivyo kulipwa jumla ya Sh. milioni 44.5,
pia Ofisi ya Msajili wa Hazina ilifanya tena zoezi la uhakiki mwezi Juni, 2019
kwa wafanyakazi ambao hawakujitokeza katika uhakiki wa awali ambapo jumla ya wafanyakazi 115 walijitokeza
pamoja na wasimamizi wa mirathi 22 ambao kwa ujumla wanastahili kulipwa
takribani Sh. milioni 20.7.
Dkt.
Kijaji alisema kuwa Serikali ilisimamisha uzalishaji katika kiwanda cha Nguo
Mutex mwaka 1994 baada ya kukabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mtaji na
ongezeko kubwa la madeni kutoka iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC)
Aliongeza
kuwa Kiwanda cha Mutex kilifilisiwa na hatimaye kuuzwa mwezi Machi, 1998 kwa
Kampuni ya LALAGO Cotton Ginnery and Oil
Mills, kisha Wadai, Serikali na Mfilisi waliridhia mapendekezo ya kulipa
kiasi cha Sh. milioni 161.3 kwa wafanyakazi 935 waliokuwepo kiwandani baada ya
kikao kilichofanyika Septemba 23, 2005.
Alisema
kuwa baada ya zoezi la ufilisi kukamilika, wafanyakazi 512 pekee ndio
waliojitokeza kuchukua mafao yao na wafanyakazi 423 waligoma kupokea mafao yao
kwa madai kwamba nauli ya familia na gharama za kusafirisha mizigo ni ndogo.
Wafanyakazi
hao 423 walifungua kesi katika Mahakama ya Kazi ya Tanzania na baadae Mahakama
hiyo ilitoa tuzo Juni 10, 2008 ambapo ilitupilia mbali shauri hilo na kuamuliwa
wadai waende kwa mufilisi kuchukua stahili zao.
Aidha
wadai hao walifungua shauri jingine la
maombi ya marejeo ambapo Februari, 2010 Mahakama
hiyo iliamua tena wadai waliogoma
kuchukua mafao yao waende kwa Mufilisi kama ilivyoridhiwa katika kikao cha
wadau.
No comments:
Post a Comment