Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA), Asmah Hilal (kushoto), akimkabidhi bendera nahodha wa timu ya Taifa ya vijana, Mohameduwais Abdullatif, timu hiyo imeondoka nchini kwenda Tunisia kushiriki mashindano ya Afrika ya kuogelea. (Na Mpiga Picha Wetu).
Waogeleaji
wa timu ya Taifa ya vijana wakiwa katika picha ya pamoja na wazazi, viongozi wa
chama cha kuogelea na wadau mara baada ya kukabidhiwa bendera.
Na Mwandishi Wetu
Timu ya Taifa ya vijana ya kuogelea imeondoka nchini kwenda Tunisia
kushiriki katika mashindano ya Afrika ya
kuogelea.
Timu hiyo
inajumuisha jumla ya waogeleaji wanne ambao ni Yuki Omori anayetokea klabu ya Mis Piranhas ya
mkoa wa Morogoro, Khaleed Ladha
(Mwanza), Aaron Akwenda (Bluefins) na
Mohameduwais Abdullatif wa klabu
ya Taliss-IST.
Makamu
mwenyekiti wa Chama Cha Kuogelea Tanzania (TSA), Asmah Hilal alisema kuwa waogeleaji wapo
tayari kuiwakilisha nchi
Katika mashindano
hayo ambayo yatajumuisha waogeleaji zaidi ya 1000 kutoka bara la Afrika.
Alisema kuwa
waogeleaji hao wamechaguliwa baada ya kufikia vigezo vya mashindano.
Hilal
alisema kuwa timu hiyo itakuwa chini ya mkuu wa msafara, Amina Mfaume ambaye ni
mkurugenzi wa ufundi wa TSA na kocha
mkuu Samwel Mtupo kutoka klabu ya Mwanza.
“Tunatarajia
kupata matokeo mazuri katika mashindano hayo pamoja na ugumu wake. Watanzania zaidi
ya milioni 50 wanatarajia kuona mnarejea kishujaa,” alisema Hilal.
Kocha wa
timu hiyo, Mtupo alisema kuwa wanajua ushindani katika mashindano hayo na
kufanya maandalizi kwa lengo la kufanya vyema.
“Tumejiandaa
kwa ajili ya kushindana na tunaamini tutafanya vyema. Naamini waogeleaji
waliochaguliwa ambao wana ubora wa hali ya juu, tutajitahidi kuiwakilisha nchi
vizuri,” alisema Mtupo.
Nahodha wa
timu hiyo, Mohameduwais Abdullatif alisema
kuwa wamejiandaa kwa ajili ya kushinda
na siyo vinginevyo.
“Tumefanya maandalizi kwa muda mrefu kwa lengo
la kuleta matokeo ambayo Watanzania watayafuraia, ” alisema Abdulatif.
No comments:
Post a Comment