Meneja Ufundi wa Mamlaka ya Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga UWASA) Mhandisi Rashidi Shaban akizungumza na waandishi wa habari leo.
Mafundi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga UWASA) wakiwa kazini kama wanaavyooekana
Fundi kutoka Idara ya Ufundi Tanga Uwasa Kitengo cha Maji Taka Sikujua Shabani wa pili kutoka kulia akionyeshwa kitu na mafundi.
Eneo la barabara ya sita ambapo bomba limeharibika lenyewe kutokana na udhaifu maji yamepita mengi na limeshindwa kuhimili msukumo wa maji.
Na Mwandishi Wetu
Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga UWASA) wameeleza sababu za uwepo wa changamoto ya mtandao wa majitaka inatokana na uchakavu wa mabomba kuwa yamelazwa siku nyingi na mengi yakiwa ya zege na udongo.
Changamoto imesababisha uzibaji na utirishaji wa majitaka katika baadhi ya maeneo ya makazi hivyo kusababisha malalamiko kwa wateja.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii Meneja Ufundi wa Mamlaka hiyo Mhandisi Rashidi Shabani alisema Tanga Uwasa imejipanga kutatua changamoto hiyo kwa kufanya ukarabati kwa awamu katika maeneo korofi ili kuondoa kero hiyo.
Changamoto ya mfumo wa majitaka imeonekana katika eneo la barabara ya sita na ishirini ambapo ilisababishwa na kubanjika kwa bomba hilo kutokana na msukumo mkubwa wa maji hivyo kupelekea mafuriko ya majitaka kwa maeneo mengine. kuna bomba limeharibika lenyewe kutokana na udhaifu maji mengi kupita na limeshindwa kuhimili msukumo wa maji hayo.
Alisema kwamba tatizo hilo limekutokana na umri wa mabomba hayo yaliyopo ardhini mengi yamekuwa mabovu na hayawezi kuhimili maji mengi kunakosababiswa na watu kuongezeka maji yanayopita kwen ye mtandao huo yamekuwa mengi kulinganisha na uwezo wa kuhimili mabomba hayo kutokana umri yaliyokwa nayo
Mhandisi Shabani alisema kwenye eneo la barabara ya sita kuna bomba limeharibika lenyewe kutokana na udhaifu maji yamepita mengi na limeshindwa kuhimili msukumo wa maji.
“Hivyo sisi kama Tanga UWASA tumejipanga kufanya ukarabati tayari kijiko kipo eneo la tukio kimeshaanza uchimbaji huku akiwaomba wananchi wawavumilie ndani ya siku mbili kwenye eneo la barabara kwa sababu ya kufanyia huo ukarabati”Alisema
Alisema kwamba wanaamini ndani ya siku mbili zijazo takuwa wamemaliza kazi
kubwa eneo hilo
“Lakini pia tutatumia ndani ya siku saba a au nane kukamilisha huduma hii hivyo wananchi wanaotumia barabara hii wapite pembeni kwa sababu hiyo ni hatari kwa afya zao kutokana na maji taka”Alisema
Naye kwa upande wake fundi kutoka Idara ya Ufundi Tanga UWASA kitengo cha Maji Taka Sikujua Shabani alisema tatizo lilpotokea mara moja wameanza kazi kwani maji taka yanapomwagika ni athari kwa wananchi.
Hata hivyo alisema kwamba wameendalea kuwaelimisha wananchi kuwa wavumilivu kwani wao hivi sasa wanalishughulikia tatizo hilo ili hali yake iweze kurudi kawaida.
No comments:
Post a Comment