Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika ukumbi wa ofisi ndogo za wizara ya kilimo Jijini Dodoma, leo tarehe 13 Septemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo).
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akizungumza wakati wakati wa kikao kazi kilichoitishwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga kukutana na watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika ukumbi wa ofisi ndogo za wizara ya kilimo Jijini Dodoma, leo tarehe 13 Septemba 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo-Dodoma
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameipa
wiki moja Tume ya Taifa ya umwagiliaji kutengeneza mikakati ya kutengeneza
mabwawa ya kukinga maji ya mvua ili kuwasaidia wakulima kuwezesha kilimo cha
umwagiliaji kukua.
Mhe Hasunga ameyasema leo tarehe 13 Septemba 2019
katika ukumbi wa ofisi ndogo za wizara ya kilimo Jijini Dodoma alipokuwa
akizungumza kwenye kikao kazi na watumishi wa Tume huyo.
Waziri Hasunga amesema kuwa wizara hiyo ina
matarajio ya kutumia fursa ya mradi mradi wa
umeme wa maporomoko ya maji ya Mto Rufiji (RHPP) utakaozalisha megawati
2115, kea ajili ya kilimo cha umwagiliaji ambapo inatajwa kuwa kuna zaidi ya
Hecta 150,000 zinazofaa kea ajili ya umwagiliaji.
Mhe Hasunga amewataka watendaji hao wa Tume ya
Taifa ya Umwagiliaji kuhakikisha kuwa wanampatia mipango na mkakati wa namna
gani baada ya umeme kuzalishwa katika eneo lile, yale maji yatatumika yote
katika umwagiliaji na hecta zote zile zianze uzalishaji.
‘’Ninawapa wiki moja hakuna muda mwingine wa
kufanya hivyo kwa sababu niliwapa mienzi minne hamjafanya hivyo’’ Alisema Mhe
Hasunga
Aidha, Waziri Hasunga ametoa siku tatu kumpatia
taarifa za utendaji kazi wa miradi ya umwagiliaji katika mikoa minne yaani
Tabora, Katavi, Rukwa, na Songwe iwapo kuna miradi inayofanya kazi na isiyofanya
kazi.
Kilimo cha umwagiliaji kimekuwa kikisisitizwa na
serikali kwani ni kilimo kisichotegemea mvua hivyo kuwa na matarajio ya kuvuna
mazao kwa wingi.
Umwagiliaji ni mtindo wa kilimo wa kupeleka maji kwa mimea shambani pasipo mvua ya kutosha, hutumiwa katika maeneo yabisi au wakati mvua ni kidogo. Katika nchi baridi unatumiwa pia kwa kusudi la kulinda mazao dhidi ya jalidi.
No comments:
Post a Comment