HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 21, 2019

TATIZO LA MAJI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM KUWA HISTORIA - PROF. NDLICHAKO

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako (wa pili kulia), akipata maelezo kutoka kwa msimamizi wa ukarabati wa majengo ya Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia (CoET), Prof. Aloyce Mayo, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya ukarabati wa mabweni mawili ya wanafunzi pamoja na mfumo wa kusambaza majisafi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). (Picha na Francis Dande).
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako (katikati). 
Kukagu ukarabati.

  Waziri akiangalia miundombinu ya ukarabati wa bomba la kupitisha majisafi.


 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akiangalia mabomba ya kupitisha majisafi.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akikagua mabomba yatakayotumika katika kukarabati mfumo wa majisafi.
 Na Mwandishi WetuWaziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, amesema mabweni mawili ya wanafunzi maarufu “hall 5 na hall 2 “katika Chuo kikuu cha Dar es salaam yaliyokarabatiwa  yatachukua wanafunzi  788 .

Prof. Ndalichako amesema hayo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya ukarabati wa Mabweni, Vyumba vya mihadhara na Ofisi ya Ndaki ya Uhandisi Katika Chuo hicho.

Waziri huyo amesema mabweni hayo, yanakarabatiwa na Serikali kwa Shilingi za Tanzania zaidi ya Bilioni 4.5, ambapo ukarabati huo umehusisha  kuweka upya mifumo ya maji safi na taka, mifumo ya umeme, kuwekwa upya makabati na milango mipya, madirisha  uwekaji vigae vipya vya ukutani na uwekaji “lift” mpya.

Ukarabati huu wa mabweni hayo yaliyojengwa mwaka 1965 ulianza mwaka 2018 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Oktoba, 2019 na   unatekelezwa na Mkandarasi SUMA JKT- na kusimamiwa na  kurugenzi ya milki ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Waziri Ndalichako ameelezea kuwa ukarabati huo mkubwa wa mabweni hayo unafanyika kwa mara ya kwanza toka yalipojengwa baada ya kusitisha utumiaji kutokana na uchakavu.

Waziri Ndalichako amepongeza kasi na ubora wa kazi ya ukarabati huo, huku akipongeza hatua ya chuo Kikuu kutumia wataalamu wake wa ndani kusimamia kazi za ukarabati katika chuo hicho. 


“Nimefurahishwa na kazi hii ni bora na  kasi ya kazi ya ukarabatiwa mabweni haya kwani  yataongeza uwezo wa chuo kutoa huduma ya Malazi kwa wanachuo zaidi ya 11,100. Naagiza uongozi mko hapa  maagizo kwa hakikisheni ukarabati wa mabweni haya na majengo katika Ndaki ya Uhandisi unakamilika kabla ya kufunguliwa Chuo Novemba  ili isiwe bugudha kwa wanafunzi, Mwaka huu ”

Akimkaribisha Waziri wa Elimu, Makamu Mkuu wa  Chuo Cha Dar es salaam Profesa  Wiliam Anangisye ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano na Waziri wa Elimu kwa kutekeleza kwa vitendo azma ya kuboresha imiundombinu ya chuo hicho ili kuhahakikisha vijana wanapata elimu katika mazingira bora.

Makamu Mkuu huyo amemuhakikishia  Waziri Ndalichako kuwa Chuo kitasimamia na kuhakikisha kazi zinazoendelea zinakamilika kwa wakati .

“ Tunaishuruku serikali ya Awamu ya Tano na wewe Mheshimiwa kwani maendeleo haya ni maono ya Serikali na yanatekelezwa na serikali , nasi tunakuhakikishia pia kuendelea kutunza miundo mbinu hii na kutumia mapato ya ndani kuyaendeleza”

Nae Dr liberato Haule Mkurugenzi wa Mipango Uwekezaji na Maendeleo akisoma taarifa ya maendeleo ya miradi amezungumzia ukarabati wa majengo ya Ndaki ya Uhandisi kuwa umefikia asilimia 45 na kuwa utagharimu shilingi bilioni  1.5  .

“ Napenda kutoa taarifa kuwa mradi wa ukarabati wa majengo ya Ndaki ya Uhandisi unahusisha  majengo ya ofisi na madarasa, nyumba za wafanyakazi na bweni moja lililopo kitalu G.  nikuhahakikishie Mh Waziri kuwa mataraji yetu ni kuwa kazi itakamilika kwa wakati uliopangwa Novemba  mwaka huu“

Nae Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi (DARUSO) Bi. Jackline Ndombele, ameishukuru serikali kwa ukarabati mkubwa unaoendelea  hall 5 na hall 2 na kwamba utasaidia sana kuongeza idadi ya  wanafunzi wanaokaa chuo, kwani kwa sasa wengi wanakaa nje ya Chuo.

No comments:

Post a Comment

Pages