Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari, akizungumza na waandishi wa habari.
NA
SULEIMAN MSUYA
KAMPUNI
ya Tigo Tanzania imesema inaendelea kupanua wigo wa huduma zake kwenye maeneo ya
vijijini ili kuchochea ukuaji wa uchumi, maendeleo na mawasiliano nchini.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Mkuu wa Tigo Tanzania Simon Karikari wakati
akiwasilisha mada kwenye mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya Tehama, Habari,
Uchukuzi na Hali ya Hewa kutoka nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
(SADC), ulimalizika jijini Dar es Salaam.
Karikari
alisema Tigo imefikia asilimia 90 ya Watanzania kwa kutoa huduma mbalimbali
kama mawasiliano, kifedha na inteneti hali ambayo inasaidia jamii kuwasiliana
kwa urahisi.
“Nimewaeleza
waheshimiwa mawaziri kuwa tumefanikiwa kufikia Watanzania kwa zaidi ya asilimia
90 kwa sasa Tigo ni ya pili kwa hapa nchini kwa kutoa huduma bora,” alisema.
Alisema
mikakati yao ni kuhakikisha nafasi ya pili ambayo wanashika kwa kutoa huduma za
simu nchini inabakia na baadae kuja kuwa viongozi kwa utoaji wa huduma hizo
nchini.
Aidha,
alisema mikakati yao itafanikiwa kwa haraka hasa kutokana na mchango wa Mfuko
wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), kutumia ruzuku wanayopata kupitia makampuni ya
simu kusambaza mikonga ya mawasiliano nchini.
Alisema
kinachofanywa na UCSAF kwa kutoa ruzuku kinapaswa kuigwa na nchi za SADC ili
kuhakikisha huduma ya mawasiliano inatakapaa kila kona ya nchi wanachama kama
ilivyo Tanzania.
Mkurugenzi
huyo alisema iwapo mfumo wa UCSAF ukipata nafasi katika nchi nyingine ni dhahiri
mitandao ya simu katika nchi hizo itasambaa kama Tigo ilivyo samba.
Kwa
upande wake Mtaalam wa Uhusiano wa Huduma za Wateja Tigo Business, Joachim
Chuwa alisema wao wanaendelea kubuni teknolojia mbalimbali ili huduma za
mawasiliano iwe na wigo mpana.
Chuwa
alisema hivi sasa wamekuja ubunifu wa tekonolojia inteneti ya kisasa ya ‘Home Inteneti
na Ofice Intenet’ ambazo zimeanza kufanya vizuri katika soko.
No comments:
Post a Comment