Na
Ibrahim Yassin, Songwe
VIJANA
774 wamehitimumafunzoyaukakamavuka tikakambiyajeshikikosi cha 845 KJ
kilichopo Kata ya Itaka wilayani Mbozi mkoani Songwe huku wakitakiwa
kutoyatumia vibaya mafunzo hayo kwa kufanya fujo badala yake wametakiwa
kuwa wazalendo kwa kulitumikiaTaifa hili.
Hii ni mara ya kanza kwa kambi hiyo ya Jeshi
la kujengaTaifalililopo kata ya Itaka wilayani Mbozi mkoani Songwe kutoa mafunzo
kwa vijana 774 ambao wamehitimu mafunzo yao ya ukakamavu na kupewa nasaa
mbalimbali ikiwemo y auadirifu na uzalendo kwaTaifa.
Filimon
Mahenmge mkuu wa kambi hiyo alisema vijana hao walianza mafunzo hayo wakiwa 780
kat ya hao wavulana 620 na hivi leo waliohitimu ni 774 kati ya hao wavulana 615
hivyo vijana 6 hawakushiriki mafunzo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya
utoro.
Alisema
vijana hao wameiva vizuri ndani ya miezi mitatu hivyo anaamini huko watako
kwenda watakuwa ni mabarozi wazuri katika kulitumikia Taifa na kuwa wazalendo
kwa nchi yao na hata watakaoendelea na masomo vyuoni watafanya vyema zaidi.
Anchilla
Kagombola muwakilishi wa mkuu wa jeshi la kujenga Taifa nchini,alisema ni kuu
ya serikali kupitia Jeshi la kujenga Taifa ni kuwakusanya vijana pamoja na
kuwafundisha mbinu za kijeshi pamoja na ukakamavu na kuwajenga kimaadili ili waweze kulitumikia
Taifa hili la uadirifu.
John
Palingo mkuu wa wilaya ya Mbozi aliyekuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa
mafunzo hayo ,amewaasa wahitimu hao kutoyatumia vibaya mafunzo waliyo yapata
kwa kufanya vurugu mitaani na badala yake wametakiwa kuyatumia vyema kwa kuwa
waadilifu na kioo kwa jamii.
Alisema
adui namba moja wa serikali hii ni rushwa,ufisadi na mambo mengine maofu,hivyo
anaamini mafunzo waliyoyapata vijana hao wataenda kupingana na vitendo hivyo na
ndiyo maana muasisi wa Taifa Mwl ,Julius Nyerere aliamua kuanzisha kitengo hiki
kwa ajili ya kuwapika kimaadili vijana ili waweze kuwa viongozi bora.
Ayoub
Majid mhitimu wa mafunzo,alisema kupitia mafunzo hayo wamejifunza mambo mengi
ya ukakamavu na mbinu za kijeshi,hivyo anaamini atauwa barozi mzuri huko
aendako na kuwahakikishia viongozi waliowapa nasaa kuwa ushauri wao watautumia
vyema.
Njegela
Maganda mhitimu wa mafunzo,alisema kutokana na umuhimu wa mafunzo hayo aliiomba
serikali kuongeza muda ili waweze kuwa wakakamavu zaidi kwani muda wa miezi
mitatu alisema hautosho licha ya kuwa tayari wamepata mafunzo yote muhimu.
Rameck
Iromo Mhitimu wa Mafunzo,alisema mafunzo yalikuwa mazuri hivyo aliiomba
serikali kutatua changamoto zilizopo kwenye kambi hiyo ikiwemo kusogeza maji
karibu,kuongeza nyumba za watumishi pamoja na mabweni ombi ambalo lilikubaliwa
na mkuu wa wilaya hiyo.
No comments:
Post a Comment