HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 09, 2019

MBWA MWENYE KICHAA AJERUHI WATU 18 BUKOBA

Na Lydia Lugakila, Bukoba

Wananchi katika Kata ya Katoro Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera wamefanikiwa kumuua Mbwa aliyekuwa na kichaa na kusababisha kuwajeruhi kwa kuwang’ata wananchi 18.

Taarifa hiyo imetolewa Septemba 8, 2019 na Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, Innocent Mzungu, na kusema kuwa mbwa huyo amekuwa kero kwa kuwang’ata wananchi 18 na kusababisha watoto na watu wazima kuamua kujifungiana ndani masaa yote huku wanafunzi wakishindwa kwenda shule ili kukwepa madhara hayo.

Katika taarifa hiyo mzungu amesema kuwa mbwa huyo alifanya madhara hayo kati ya Septemba 5 na 6 mwaka huu na kufanya idadi hiyo kuwa 18.

Mtendaji huyo amesema kutokana na kero hiyo yenye madhara makubwa ndipo wananchi wa kijiji cha Ruhoko wamefanikiwa kumuua mbwa huyo na kutolewa tamko kwa kila mwananchi aliyefuga mbwa na paka kuwapeleka wanyama hao kuapatiwa chanjo Sepemba 9 mwaka huu huku watakaokiuka tamko hilo kutozwa faini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera mh. Hashimu Murshid Ngeze ili kujua hatima ya tukio hilo ambapo amesema kuwa Kipindi cha mwezi jana tukio hilo liliikumba kata ya Rukoma wilayani humo ambapo baadhi ya wananchi waliwang’ata na mbwa mwenye kichaa jambo liliwafanya viongozi hao kukaa kwa maana ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo pamoja na mkuu wa idara ya mifugo na kukubaliana kwa pamoja kuwa mbwa ambao wanabainika kuwa na kichaa wachanjwe na kuwa hivi karibuni madawa ya kuchanja yaliletwa na tayari zoezi la kuchanjwa kwa mbwa hao linaendelea ndani ya wilaya hiyo

‘’Mwaka 2018 mbwa baadhi walichanjwa lakini wananchi akiwemo wafugaji wenyewe walikaidi kupeleka mifugo hiyo kupata chanjo natoa agizo kila mbwa achanjwe’’ amesema,

Ametoa wito kwa wananchi wanaofuga mbwa kuhakikisha wale ambao wanasadikika kuwa na kichaa wafungiwe ndani wakati zoezi la kuwachanja likiendelea

Katika hilo amewataka watendaji wa kata kuhakikisha wanashirikiana na wananchi ili kufanikisha zoezi hilo na kuwa ni agizo la lazima kila mbwa kupatiwa chanjo ili kuepusha madhara katika jamii.

No comments:

Post a Comment

Pages