HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 22, 2019

Vodacom yalipa gawio la bil. 54.5/-

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Vodacom,  Ali Mufuruki, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano wa wanahisa wa kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Hisham Hendi. (Picha na Francis Dande). 

NA MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya mawasiliano ya simu za mikononi inayoongoza Tanzania ya Vodacom Tanzania PLC, jana ilitangaza faida ya mwisho wa mwaka ya kiasi cha bilioni 90.2/- kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ulioishia Machi, mwaka huu.

Mbali ya mafanikio hayo, Vodacom inayojivunia kuwa mtandao wenye kasi zaidi nchini inajivunia thamani iliyovuna kipindi cha miaka ya karibuni ikiwemo bil. 54.5/- zilizolipwa gawio kwa wanahisa wake.

Taarifa ya Kampuni hiyo kwa vyombo vya habari, ilisema jana ya kuwa ongezeko hili limechangiwa na kuongezeka kwa mapato ya huduma yanayofikia bil. 1018.9/- ikiwa ni matokeo ya kukua na kuimarika kwa mapato ya huduma za M-pesa, ununuzi wa Intaneti na mapato ya ujumbe wa simu.
Aidha, Vodacom imepata wateja wapya wapatao milioni 1.2 katika mwaka huu wa fedha jambo ambalo linaongeza idadi yake ya wateja kufikia milioni 14.1.

Katika mwaka huu wa fedha kampuni ya Vodacom ilifanya uwekezaji mkubwa wa zaidi ya TZS bilioni 171.4 sawa na asilimia 16.7% ya Mapato katika kupanua mtandao wake, kuongeza maeneo yanayopata mtandao wa 4G katika miji mikubwa nchini, kuongeza uwezo na kuboresha mtandao kuweza kutoa huduma ya data ya kiwango cha juu kwa wateja.

Wakati hu huo, kiasi cha shilingi bilioni 59, zimewekezwa katika mishahara, mafunzo na maendeleo ya wafanyakazi wake wa kudumu wapatao 548 pamoja na kutoa ajira isiyo ya moja kwa moja kwa zaidi ya Watanzania 127,000.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Kampuni ya Vodacom, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya Vodacom  Ali Mufuruki alisema: 

“Kampuni ya Vodacom pia inajivunia uwekezaji wake katika jamii ambao una thamani ya jumla ya sh. trilioni 1.1. Hizi ni fedha zilizochangiwa katika uwezeshaji wa jamii kupitia kodi, ada za udhibiti katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita ambapo malipo ya zaidi ya Sh. trilioni 0.4 yalifanyika katika mwaka 2019 peke yake.”

“Ukuaji katika sekta ya mawasiliano imekuwa wa pole pole katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni. Tukiwa kama watendaji muhimu katika sekta hii, tunajivunia kuwa chanya katika ukuaji wa sekta hii,” alihitimisha Mufuruki.

No comments:

Post a Comment

Pages