Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb)
akimkabidhi zawadi ya kinyago cha umoja Balozi wa Rwanda hapa Nchini Mhe.
Eugene Kayihura ambaye amemaliza muda wake wa Utumishi hapa Nchini. Balozi
Kayihura amekuwa Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano.
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb)
akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Rwanda hapa Nchini Mhe. Eugene
Kayihura mara baada ya kupata chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa ajili ya
kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa Utumishi hapa Nchini. Balozi Kayihura
amekuwa Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano.
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb)
akiagana na Balozi wa Rwanda hapa Nchini Mhe. Eugene Kayihura mara baada ya
kupata chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza
muda wake wa Utumishi hapa Nchini. Balozi Kayihura amekuwa Balozi wa Rwanda
Nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano.
Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amemuaga Balozi
wa Jamhuri ya Rwanda nchini Mhe. Eugene Kayihura, ambaye amemaliza muda wake wa
uwakilishi.
Akiongea wakati wa hafla
hiyo iliyofanyika jana Dar es Salaam Prof. Kabudi alimshukuru Balozi Kayihura
kwa kumaliza muda wake wa uwakilishi na kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya
ya kudumisha mahusiano kati ya Tanzania na Rwanda katika kipindi chake cha
uwakilishi.
Aidha, Mhe. Waziri alielezea
kwamba yapo maeneo ambayo nchi hizi mbili zitaendelea kushirikiana kwa ukaribu
na maeneo mengine Tanzania itaendelea kubadilishana uzoefu na Rwanda ikiwemo
huduma za kusambaza madawa maeneo ya vijijini na TEHAMA.
Kwa upande wake, Mhe.
Balozi Kayihura aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kumpa ushirikiano wa
kutosha wakati wa kipindi chake cha uwakilishi hapa nchini.
Mhe. Balozi alielezea kufurahishwa na uhusiano mzuri uliopo baina ya
nchi hizi mbili na alipongeza hatua mbalimbali ambazo Serikali ya Tanzania
imeendelea kuzichukua katika kuimarisha mahusiano hayo. Aliongeza kwamba hatua
hizo zimefanikisha idadi ya wafanyabiashara wa Rwanda kutumia bandari ya Dar es
Salaam kusafirisha mizogo yao kuongezeka hadi kufika asilimia 98.
No comments:
Post a Comment