HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 18, 2019

WATAKAOHUJUMU VYANZO VYA MAJI KAGERA KUCHUKULIWA HATUA KALI

Ofisa Maji Mkoa wa Kagera, Mberwa Olengeire.

Na Lydia Lugakila, Bukoba

Ofisa Maji kupitia Ofisi Ndogo ya Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera amejipanga kuhakikisha jamii inapewa elimu juu ya kuhifadhi, kulinda na kuthibiti uchafuzi katika vyanzo vya maji ili viweze kudumu kwa matumizi endelevu huku akitaja watakao kiuka sheria ya vyanzo hivyo  kufikishwa mahakamani au kutozwa faini.

 Ofisa Maji Mberwa Olengeire ametoa kauli hiyo leo Septemba 18, 2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Olengeire amesema kuwa licha ya elimu kuendelea kutolewa wapo baadhi ya Wananchi wamekuwa wakifanya kuvunja sheria na kanuni katika kulinda , kutunza na kuhifadhi vyanzo hivyo kwa makusudi huku wakijua kuwa kwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria.

Amesema Uwepo wa vyanzo vya maji vilivyo salama usaidia miradi ya kusambaza maji kuwa yenye mafanikio makubwa.
 ‘Tuungane na Rais wa Jamhuri ya Muunagano wa Tanzania katika kuelekeza Tanzania ya Viwanda kwa kuvitunza na kuvilinda nyanzo vya maji ziwa Victoria ndio uchumi wetu tunapaswa kuvilinda kwa hiyo atakayekiuka maagizo ya viongozi wa nchi yetu atafikisha mahakamani na faini juu yake’ alisema.

Ofisa huyo ameongeza kuwa kila mtu anapaswa kumlinda mhusika yeyote anayeharibu chanzo cha maji na kutoa taarifa ili awajibishwe vilivyo na kuwa wananchi wanatakiwa kuacha kulima karibu na vyanzo vya maji, kukata miti ambayo ni rafiki wa vyanzo vya maji, kupanda miti isiyo rafiki na maji katika vyanzo hivyo kwani shughuli hizo ni uharibifu wa vyanzo hivyo.

Amesema elimu itaendelea kutolewa na kuwa watakaokahidi watapelekwa mahakamani au kutozwa faini huku akiitaka jamii kushirikiana na bodi za mazingira katika uhifadhi wa mazingira  kutunza na kuviendeleza vyanzo vya maji vilivyopo.

Amesema Bodi hiyo ni Taasisi inayoshughulika na masimamizi ya usimamizi wa raslimari za maji ikiwemo kulinda na kuthibiti uchafuzi wa vyanzo vya maji katika bonde la ziwa Victoria na eneo lote muelekeo wa maji ambayo uingia katika ziwa Victoria ambapo  ametaja  Bonde la ziwa Victoria kuigusa mikoa 5 ikiwemo ni Mara, Mwanza, Simiyu, Kagera Na Shinyanga.

Aidha amesema jamii itambue sekta ya maji kuwa ni sehemu muhimu hivyo ni vyema kulinda vyanzo hivyo na kuvitunza kwa kuzuia ukataji miti, kulima kwenye vyanzo vya maji, pamoja na shughuli zote ambazo haziruhusiwi kufanyika ndani ya  mita 60.

No comments:

Post a Comment

Pages