HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 07, 2019

Serikali ya Marekani Kupitia Development Credit Authority (DCA) Imesaini Mkataba na Benki ya Amana

 Naibu Mkurugenzi wa USAID katika Idara ya Afrika, Dk. Diana Putman (kushoto) na Mkurugenzi wa Benki ya Amana, Dk. Muhsin Salim Masoud, wakibadilishana hati baada ya kusaini mkataba wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 10  wenye lengo la kuimarisha uwezo wa benki hiyo kutoa fedha kwa shughuli zinazohusiana na kilimo na biashara ndogondogo na za kati na kwa biashara zinazomilikiwa na wanawake na vijana nchini.
 Naibu Mkurugenzi wa USAID katika Idara ya Afrika, Dk. Diana Putman (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Benki ya Amana, Dk. Muhsin Salim Masoud (wa pili kulia), wakisaini mkataba wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 10  wenye lengo la kuimarisha uwezo wa benki hiyo kutoa fedha kwa shughuli zinazohusiana na kilimo na biashara ndogondogo na za kati na kwa biashara zinazomilikiwa na wanawake na vijana nchini.
  Mkurugenzi wa USAID/Tanzania, Andrew Karas (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Amana, Dk. Muhsin Salim Masoud (wa tatu kulia), wakizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kusaini mkataba wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 10  wenye lengo la kuimarisha uwezo wa benki hiyo kutoa fedha kwa shughuli zinazohusiana na kilimo na biashara ndogondogo na za kati na kwa biashara zinazomilikiwa na wanawake na vijana nchini. (Picha na USAID)).


Dar es Salaam: Oktoba 7, 2019, Serikali ya Marekani, kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), imesaini mkataba wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 10 na Benki ya Amana. Lengo la DCA ni kuimarisha uwezo wa benki hiyo kutoa fedha kwa shughuli zinazohusiana na kilimo na biashara ndogondogo na za kati na kwa biashara zinazomilikiwa na wanawake na vijana nchini Tanzania.

Wakati wa hafla hii, Dk. Diana B. Putman, Naibu Mkurugenzi wa USAID katika Idara ya Afrika alisema, “Mkataba huu umekusudia kuimarisha uwezo wa Benki ya Amana kutoa fedha kwa Kilimo biashara nchini Tanzania. Hivyo, tunatarajia utachangia katika ukuaji endelevu wa biashara zinazohusiana na kilimo.”

Mbali na kufadhili upatikanaji wa mikopo, mkataba huu umeongeza upatikanaji kwa wateja na mikoa ya Tanzania, ikiwemo Zanzibar. Wakati USAID inashirikiana na benki za Kiislamu katika maeneo mengine duniani, mkataba na Benki ya Amana ni wa kwanza kwa Benki ya Kiislamu
Kusini mwa Jangwa la Sahara. 
Serikali ya Marekani inaunga mkono maendeleo ya biashara na mchango wa sekta binafsi katika kuchangia maendeleo ya Tanzania na uwezo wa kufikia hadhi ya kujitegemea.

No comments:

Post a Comment

Pages