HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 07, 2019

BENKI YA CRDB YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA 2019 KWA KISHINDO

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akiwahudumia baadhi ya wateja wa benki hiyo tawi la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja.




























NA MWANDISHI WETU

MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, amewaongoza baadhi ya watendaji wa benki hiyo kugawa chai kwa wateja wao.

Akizungumza akiwa kwenye tawi la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja, Nsekela alisema ni wiki muhimu kwa wateja wa CRDB.

Alisema ni wiki ya viongozi wa benki hiyo kutoka matawi yote kuwafuata na kuwahudumia wateja kwa upendo chini ya kaulimbiu ya 'Ulipo tupo kukupa Magic'.

"Hii ni wiki ya huduma kwa wateja duniani kaulimbiu ya dunia ni 'The magic of service' na sisi benki yetu tunashiriki kwa kuwahudumia wateja wetu.

"Tunawaambia ulipo tupo kukupa Magic. Tumeandaa vitu vingi vizuri naamini wateja wetu watafurahia," alisema Nsekela.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, TullyEsther Mwambapa, alisema wafanyakazi wa benki hiyo watafanya shughuli za kijamii kwa kushtukiza na kuwashukuru wateja wao.

"Ni wiki hii ya huduma kwa wateja, tunaitumia kushukuru wafanyakazi wetu kwa huduma wanazozitoa na kushukuru wateja wetu kwa kutuchagua.

"...Tutawafikia na kuwahudumia wateja wetu kwa kuwashtukiza hivyo wajiandae kwa mambo mazuri," alisema Mwambapa.

No comments:

Post a Comment

Pages