NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
MILVIK
Tanzania kwa kushirikiana na Tigo Pesa, Resolution na Mo wameshinda
tuzo ya huduma ya Bima yenye ubunifu zaidi kupitia huduma yake ya Bima
Mkononi.
Meneja
Mkuu wa Milvik, Berengere Lavisse, alisema wanajivunia kutoa huduma
rahisi na nafuu kwa wateja wa kipato cha chini kwa ushirikiano na Tigo
Pesa, Resolution na Mo.
"Kupitia
bima yetu mpya ya kulazwa na watoto, wazazi wanaweza kuwalinda watoto
wao kwa matibabu ya kulazwa kwa shilingi 750 tu kwa mwezi kwa kila
mtoto, kwa kutumia simu zao, bila kujaza fomu za makaratasi na kwa mfumo
rahisi wa malipo kupitia Tigo Pesa.,"
"Tunawashukuru
wateja wetu ambao wameendelea kutuamini katika kulinda hatima za
familia zao na tunatarajia kuwaletea huduma zenye ubunifu zaidi katika
mwaka 2020.”alisema Lavisse
Alisema
kuhusu bima mkononi kuna huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na Bima
mkononi ya kulazwa kwa sh 1500 kwa mwezi, Bima mkononi ya ajali binafsi
shilingi 1,000 na bima mkononi ya maisha shilingi 1,500, au kifurushi
chenye bima zote kiitwacho bima mkononi Faraja Yangu.
Mnamo
mei mwaka huu, Milvik ilizindua mfumo mpya wa malipo unaowezesha wateja
kukatwa malipo kila mwezi kutoka kwenye akaunti zao za Tigo Pesa, na
kuifanya Bima Mkononi kuwa huduma ya gharama nafuu na rahisi kutumia kwa
watumiaji wa kipato cha chini.
Imeelezwa
kuwa wateja wanaweza kudai fidia ya shilingi 40,000 kwa kila usiku
watakaolazwa hospitali, shilingi 3,000,000 iwapo mteja atapatwa na
umauti au ulemavu wa kudumu kutokana na ajali, na shilingi 1,000,000 kwa
umauti wa sababu yoyote.
Kutokana
na ushirikiano wake na Tigo, Milvik ina kituo cha huduma kwa wateja
jijini Dar es Salaam kinachowawezesha kuwafikia watumiaji kote nchini
hivyo kukuza wigo wa huduma na kuendelea kutoa huduma za gharama nafuu.
Na
jinsi ya kujiunga kupitia simu yako ya mkononi kwa kupiga *148*15# au
kupitia huduma kwa wateja kwa kupiga simu ya bure 0659071001.
No comments:
Post a Comment