HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 05, 2019

TCRA kampeni ya Mnada kwa Mnada Chalinze katika utoaji wa Elimu ya Usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole

Wananchi wakiwa katika foleni ya usajili wa vitambulisho vya Taifa katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada katika Viwanja. Vya Bwilingu Chalinze mkoani Pwani.
Mwananchi akiweka taarifa za usajili katika Mnada wa Chalinze wakati Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA ikiwa imepita kwa ajili ya kutoa Elimu ya usajili wa laini kwa alama za vidole.
 

 Na Mwandishi Wetu

Wakazi wa Chalinze  na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni  ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji  kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

Kampeni tangu imeanzishwa imekwenda katika Mikoa 15 lengo kuu ni nchi nzima kufiwa na Kampeni hiyo.

Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA  Mhandisi Lawi Odiero amesema ni fursa kwa wananchi wa Chalinze na vyunga brake   katika Uwanja wa Bwilingu wajitokeze ya kujisajili laini za simu kwa alama za vidole na  huduma nyinginezo  kutokana  na kuwepo kwa mnyororo   wadau wa  mawasiliano.

Mhandisi Odiero amesema kuwa  Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa ya Wananchi kuhudumiwa hasa wakati huu usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.
Amesema muda uliopo ni miezi mitatu hivyo Wananchi wakamilishe taarifa zinazohitajika katika kujisajili laini za simu  kwa alama  za vidole.

Aidha amesema Kampeni hiyo ni kuimarisha ulinzi katika mawasiliano ya simu pamoja kufanya mawasiliano kuwa salama katika nchi.

Amesema  kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

Odiero  amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe  wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole na huduma nyinginezo za Mawasiliano hayo.
Hata hivyo Kanda ya Mashariki itapita katika wilaya zote katika mikoa mitano ya kanda hiyo ambayo Morogoro,Pwani Dar es Salaam, Lindi pamoja  Mtwara.

Amesema kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kuwaelewesha makosa ya jinai ya matumizi ya simu.

Aidha amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha NIDA.

Mhandisi Odiero amesema kuwa TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili mtumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa.

Hata hivyo amesema kuwa wananchi wajitokeze katika kujisajili kwa alama za vidole kabla ya Desemba 31.

"TCRA tumejidhatiti katika kuwafikia  wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo" amesema Kavishe.

Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa mwitikio umekuwa mkubwa kwa Wananchi kutaka vitambulisho kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole.

Masasi amesema kuwa Wananchi wa watumie Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA kupata elimu na baada ya kuisha Mnada sehemu husika waende katika mamlaka husika kupata vitambulisho.

Ameongeza kuwa watahakikisha kila mwananchi anajisajili kwa alama za vidole kwani Watu wana haki ya kuwa na mawasiliano ya simu.

No comments:

Post a Comment

Pages