BAADA ya zuio la
mwezi mmoja Mfuko wa uwekezaji wa ‘Bond Fund’ unaoendeshwa na Kapuni ya UTT
AMIS umerejea sokono kwa wateja kupata fursa ya kununua vipande vya hati
fungani kuanzia Novemba 16 mwaka huu.
UTT AMIS
inasimamia takribani mifuko mitano ya uwekezaji ambayo ni Umoja, Wekeza Maisha,
Watoto, Jikimu na Ukwasi na sasa mfuko wa sita ni ‘Bond Fund’ wenye lengo la
kutoa gawio, kulingana na faida itakayopatikana pamoja na kukuza mtaji kwa
wawekezaji wa muda mrefu.
Akizindua awamu ya
pili ya mauzo ya vipande vya mfuko wa Bond, Mkurugenzi Mkuu wa UTT AMIS, Simon
Migangala amesema mauzo ya awamu ya kwanza yalikuwa mazuri, kwa ushiriki wa
wawekezaji karibia 2000, huku kiasi kilichokusanywa ni Tsh, Bilioni 15.9.
“Mifuko ya
uwekezaji wa pamoja huwa ina mauzo ya awali halafu baada ya kipindi cha mwezi
mmoja huwa tunafungua tena, tukisha fungua sasa yanakuwa ni mauzo endelevu,
awali tulifungua Septemba 16, mauzo yakaenda hadi Oktoba 15.
“Mauzo yalienda
vizuri sana, wawekezaji wengi walijitokeza
karibia 2000 walishiriki kununua vipande vya mfuko wa ‘Bond Fund’ na
kiasi ambacho kimekusanywa katika kipindi hicho TSh, Bilioni 15.9, Wawekezaji
tunawashukuru wameweza kuitikia wito kwa kiasi kikubwa sana.
“Kuanzia Novemba
16, kulingana na ruhusa ambayo tumepewa na masoko ya mitaji na dhamana,
tunafungua mauzo tena, kwaiyo kwa wawekezaji ambao walikosa nafasi ya kununua
vipande vya mfuko wa ‘Bond Fund’ hapo awali sasa wananafasi ya kuweza kufanya
hivyo.”amesema Migangala.
“Baada ya mauzo ya
awali kufungwa mwezi oktoba kuna wateja ambao waliendelea kuwekeza, kuna maswali
fedha zao zitafanywaje?, Ni kwamba vipande vyao vitagawiwa kwa kutumia thamani
ya bei ya kipande ya awamu hii ya pili ya kuanzia Novemba 16.
“Pia
tunawawekezaji karibia 2000 ambao walifungua akaunti, 1415 wao waliweka pesa
katika kipindi cha mwezi wa mwanzo, lakini kuna wawekezaji 551 wao hawakuweza
kuweka pesa, kwaiyo sasa hivi ni fursa kwao kuwekeza katika mfuko kupitia zile
akaunti zao kwani bado ziko hai.”amesema Issa Wahichinenda, Mkurugenzi wa
Uwezeshaji wa UTT AMIS.
Nae Mkurugenzi wa
Tehama wa Kampuni hiyo, Sophia Mgaya amesema UTT AMIS, imeendelea kurahisisha
huduma kwa wawekezaji wao kupitia njia za Simu na Mitandao ya kijamii.
“Kwa sasa UTT AMIS
huduma zetu zinapatikana kiganjani kwa maana njia za simu, unaweza kupata
huduma hizi za kununua vipande, kufungua akaunti ama kupata taarifa ya
uwekezaji wako kupitia huduma ya *150*82# ama kwa kupakua ‘App’ yetu ya UTT
AMIS, lakini pia tumejiunganisha na mitandao ya simu, hata bila kuwa na App
yetu unaweza kununua vipande kupitia T-Pesa, M-Pesa, Airtel Money na T-Pesa.
“Lakini pia
tumeunganisha mfumo wetu na Benki ya CRDB kwa wateja wote wa CRDB wanaweza
kununua vipande kwa kupitia akaunti zao za benki ya CRDB wanazotumia.”amesema Mgaya.
Katika hatua
nyingine Mifuko mingine ya UTT AMIS ukiondoa ‘Bond Fund’ itafanya mikutanao ya
mwaka Novemba 30 na Desemba Mosi mwaka huu.
No comments:
Post a Comment