Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimetoa mafunzo ya
Siku tano kwa wafanyakazi wanataaluma wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa
(MUCE) Mkoani Iringa, jinsi ya Kupata Makala kutoka katika Tasnifu zao. (On How to turn a Thesis/Dissertation into a
Journal Article). Mafunzo hayo yalianza rasmi tarehe 2 Novemba 2019 na
yanatarajiwa kumalizika tarehe 5 Novemba, 2019.
Mkurugezi wa Kurugenzi ya Huduma kwa Umma Dkt.
Mona Mwakalinga, pamoja na Dr. Fikira Kimbokota wa Chuo Kikuu Kishiriki cha
Elimu Mkwawa wakifuatilia jambo wakati wa mafunzo hayo chuoni hapo.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma, Utafiti na Ushauri) Kikuu cha Dodoma Prof. A
Makulilo na Prof. A Mtembei wa Chuo Kikuu Dar es Salaam wakiteta jambo wakati
wa Mafunzo yanayoendelea katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa. (MUCE).
Baadhi ya wanataaluma wakifuatilia kwa makini
mafunzo ya Kupata Makala kutoka katika Tasnifu zao yaani (How to turn a Thesis /
Dissertation into a Journal Article). Yaliyoandaliwa na Kurugenzi ya Huduma kwa
Umma kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mmoja wa wanataaluma wa Chuo Kikuu Kishiriki
cha Elimu Mkwawa, akiuliza jambo wakati wa mafunzo Kupata Makala kutoka katika
Tasnifu zao. (How to turn a Thesis / Dissertation
into a Journal Article).
No comments:
Post a Comment