HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 19, 2019

FILAMU YA KASHINDE KUINGIA SOKONI NOVEMBA 29

 Mkurugenzi wa kampuni ya Lugwa Limited, Luckyness Mokiwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa uuzaji wa DVD ya filamu ya Kashinde unaotarajia kufanyika Novemba 29, mwaka huu wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani.


Na Tatu Mohamed
 
KAMPUNI ya Lugwa Limited inatarajia kuzindua uuzaji wa DVD ya filamu ya Kashinde Novemba 29, mwaka huu, mkoani Pwani.

Filamu hiyo ambayo imezinduliwa hivi karibuni ndani yake kuna wasanii wengi maarufu wakiwemo Salim Ahmed 'Gabo' Patcho Mwamba, Luckyness Mokiwa, Flora Mvungi, Grace Mapunda, Husna Sajenti, Miriam Robert pamoja Mohamed Fungafunga.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Luckyness Mokiwa alisema DVD hizo zitasambazwa na kampuni ya Steps Entertainment.

"Kama nilivyotangulia kusema hapo awali, uzinduzi tayari tulishaufanya na sasa tunaenda kuzindua uuzaji wa DVD, hivyo watu wajitokeze kwa wingi kuja kununua.

"Itazinduliw katika viwanja vilivyopo Kibaha picha ya Ndege... Na mbali na uzinduzi huu, pia kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbambali akiwemo Snura, Sister Fay na bendi mbalimbali," alisema Luckyness ambaye pia ni muigizaji Mkuu katika filamu hiyo.

Naye Gabo alisema Kashinde ni filamu ambayo imezungumzia maisha halisi ya mwanamke wa kitanzania na jitihada ambazo anapambana nazo kujikwamua kimaisha.

"Nimeiona ni filamu ya utofauti, toka kwenye kuifanya na hata nilipoambiwa niifanye ndo maana sikupinga, ni filamu nzuri kwa kweli," alisema.

Mwakilishi kutoka Kampuni ya Steps Entertainment Kambarage Ignatus alisema baada ya kutokuwepo kwa takriban mwaka mmoja, sasa wanarudi na filamu ya Kashinde.

"Tunarudi kutest mitambo kwa kusambaza filamu hii ya Kashinde, nina uhakika kila atakaye fanikiwa kuiona itabadilisha maisha yake. Hata hivyo kuanzia Januari tutaanza kupokea filamu zingine rasmi," alisema Ignatus.

No comments:

Post a Comment

Pages