HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 19, 2019

STARS JINO KWA JINO DHIDI YA LIBYA LEO

Na John Marwa 

TIMU ya Taifa, 'Taifa Stars' leo inashuka dimbani kumenyana na Libya mchezo kwa kundi J kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2021) Cameroon, katika mji wa Tunis nchini Tunisia kuanzia majira ya saa 4:00 usiku. 

Stars wanashuka kwenye mtanange wa leo wakiwa na mzuka wa ushindi walioupata hapa nyumabni Novemba 15 Uwanja wa Taifa dhidi ya Equatorial Guinea kwa mabao 2-1.

Mpambano huo wa leo unatarajiwa kuwa wenye upinzani mkubwa kutokana na Libya kupoteza mechi yao ya kwanza dhdi ya Tunisia kwa mabao 4-1 hapo hapo Tunisia. 

Stars wanahitaji kuibuka na ushindi ili kujiweka vema kufuzu fainali hizo kwa mara ya pili mtawalia baada ya kufanya hivyo katika fainali zilzopita baada ya miaka 39 walipifuzu kwa mara ya kwanza na kama watafanikiwa kufanya hivyo itakuwa ni mara tatu Tanzania kucheza fainali hizo hapo 2021 nchini Cameroon. 

Stars wanaingia kwenye kabumbu hilo wakiikosa huduma ya mchezaji mwandamizi Erasto Nyoni ambaye anauguza majeraha aliyoyapata dhdi ya Equatorial Guinea. 

Lakini pia Stars chini ya Kocha Mkuu Etienne Ndayiragije watakuwa wanahitaji ushindi wa pili mfululizo tangu alipotangazwa kuwa Kocha Mkuu na watatu mtawalia tangu ashike mikoba ya kuinoa Stars. 

Wakati Stars wakiwa wageni wa Libya, Tunisia wao wamesafiri hadi Equatorial Guinea kuwavaa katika mchezo mwingine wa kundi J. 

Hata hivyo wachezaji wa Stars wamesema wanatambua umuhimu wa kupata matokeo chanya katika mchezo huo na kuahidi kutowaangusha Watanzania usiku wa leo. 

Stars tayari imetinga hatua ya makundi kufuzu Fainali za kombe la Dunia 2022 Qatar, pia imefuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN 2020, CAMEROON).

No comments:

Post a Comment

Pages