HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 02, 2019

KATIBU MKUU RT AJIUZULU

KATIBU Mkuuwa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Wilhelm Gidabuday leo ametangaza rasmi kuachia ngazi katika nafasi hiyo.

Makamuwa Kwanza waRaisanayeshughulikiautawalawaRT,William Kalaghe alisema kuwa Gidabuday alitangaza rasmi kujiuzulu katika kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyikakwa dharura katika hoteli ya Colo jijini Dar es Salaam.

Gidabuday alithibitisha hilo leona kusisitiza kuwa hakuna shinikizo lolote lililomfanya kuchukua uamuzi wake huo, kwani amefanya hivyo kwa manufaa ya mchezo huo nchini.
 
Alisema kuwa pamoja na RT awali juzi kuwa na kikao na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, viongozi wengine wa michezo wa Serikali, lakini hakuna shinikizo lolote, kwani yeye alijiuzulu katika kikao kilichofanyika baadae juzi usiku.

Kikao cha awali cha RT na Serikali kilifanyika katika hoteli ya Slipway kuanzia saa nane mchana hadi saa mbili usiku, nabaadaekufuatianakile cha dharura pale Colo Beach.

Kikao hicho na Waziri kiliitishwa b aada ya kutokea sitofahamu ndani ya RT, ambapo Gidabuday alikuwa akisisitiza kuwa kuna mgogoro mkubwa wakati Rais wa shirikisho hilo, Anthony Mtaka kudai kuwa hakuna mgogoro wote.

Kamati ya Utendaji ya RT, imeridhia hatua hiyo ya Gidabuday na kumtakia kila la heri katika majukumu yake mengine nje ya ukatibu mkuu wa RT na kwamba itaendelea kumtumia pale itakapohitajika.

Hivi sasa, Nafasi ya Katibu Mkuu itakaimiwa na Ombeni Zavalla hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo.
 
Katika hatua nyingine, Rais wa RT, Anthony Mtaka, ameteua kamati ya wawu watatu itakayoratibu maandalizi ya Tanzania kuelekea michezo ya Olimpiki Tokyo 2020.
 
Kamati hiyo itakuwa na wajibu wa kukutana na kutoa ushauri  kwa wachezaji, rais wa RT na Kamati ya Utendaji kuelekea Olimpiki Tokyo 2020.
 
Walioteuliwa ni Wanariadha nguli, Dk. Hamad Ndee, Kanali mstaafu Juma Ikangaa na Meja mstaafu Filbert Bayi.

No comments:

Post a Comment

Pages