Waziri
wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza wakati wa uzinduzi
wa Kongamano la Pili la Utafiti na Maendeleo Endelevu la Chuo Kikuu Cha Dar es
Salaam Jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki
wakifuatilia Kongamano.
Balozi
wa Sweeden Tanzania Anders Sjoberg akizungumza na washiriki wa kongamano la
Pili la Utafiti na Maendeleo Endelevu lilizunduliwa leo Mkoani Dodoma katika
Ukumbi wa Mikutano wa LAPF.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, akipata maelezo ya utengenezaji wa Juisi ya Ndizi kwa njia ya kisasa kutoka kwa Dkt. Oscar Kibazohi (Kulia) wa UDSM baada ya uzinduzi wa Kongamano. (Picha na Francisca Swai).
Na Francisca Swai
Waziri
wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amezindua rasmi kongamano la pili la Utafiti
na maendeleo ya Endelevu la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na
Serikali ya Sweeden kupitia mradi wa SIDA/ SAREC.
Kongamano
hilo la siku mbili kuanzia tarehe 14 na 15 Novemba,2019 limefanyika Jijini Dodoma.
Kongamano
hilo, limewashirikisha wanataaluma kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa
kushirikisha wanataaluma kutoka vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi, wadau wa
maendeleo, wawakilishi kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Bunge
la Wawakilishi kutoka Zanzibar, Asasi za Kijamii, Wizara na Taasisi mbalimbali.
Lengo
la Kongamano hilo ni kuzungumzia utekelezaji wa mpango wa SIDA inayotekelezwa
na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika kipindi cha Miaka mitano 2015 – 2020,
miongoni mwa tafiti zitakazo jadiliwa ni pamoja na Kilimo-Biashara, Utalii,
Usalama wa Chakula, Sayansi ya Bahari na tafiti mbalimbali zenye kugusa maendeleo
ya wananchi.
No comments:
Post a Comment