Mkuu
wa Mkoa wa Arusha - Mrisho Gambo(kushoto) akisalimiana na mmoja wa
wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mrisho Gambo ya jijini Arusha
wakati wa hafla ya kukabidhiwa meza na viti vyenye thamani ya shilingi
10 milioni vilivyotolewa na benki ya NMB. Katikati ni Meneja wa NMB
Kanda ya Kaskazini - Aikansia Muro.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Kihaka wilayani Kilolo - Iringa wakiwa wamebeba stuli za maabara muda mfupi baada ya kukabidhiwa
na benki ya NMB.Benki ya NMB ilikabidhi meza na stuli 60 vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 10.
Wanafunzi
wa shule ya Msingi Maduma iliyoko Kata ya Maduma Wilayani Mufindi
wakishangilia madawati waliyokabidhiwa na benki ya NMB
juzi shuleni kwao.
Mkuu
wa Wilaya ya Rorya - Simon Chacha akiwa ameketi na wanafunzi wa shule
ya Msingi Minigo juzi (Jumanne) katika moja ya madawati yaliyotolewa na
benki ya
NMB ili kusadia kupunguza uhaba wa madawati shuleni hapo. Wengine ni
Kaimu Meneja wa Kanda ya Ziwa (Mwenye koti na Tai Nyeusi) – Amos Mubusi.
No comments:
Post a Comment