Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Generali Marco Elisha Gaguti, akizungumza na viongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Kagera (KCU).
Na Lydia Lugakila,
Kagera
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Generali Marco Elisha Gaguti
amewataka watumishi na taasisi zilizokopa fedha katika Benki ya wakulima ambayo ilifungwa
kuhakikisha wanarejesha fedha hizo ndani ya siku 4.
Akizungumza na viongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Kagera KCU, Chama kikuu cha
ushirika wilaya ya Karagwe na kyerwa
KDCU amesema amefuatilia na kukuta zaidi ya shilingi bilioni 2
hazijarejeshwa bado zimo mikononi mwa watumishi na taasisi hizo.
Brigedia Gaguti amesema kukopeshwa kwa fedha hizo bila
kufuata utaratibu ndo kulisababisha benki hiyo kufungwa na hivyo kuwataka
watumishi hao kutambua kuwa fedha hizo ni za wakulima.
Amesema kuwa atakayeshindwa kurejesha fedha hizo ndani ya
siku 4 anatakiwa kujisalimisha kwenye kamati ya ulinzi na usamalama ya mkoa
vinginevyo hatua kali za kisheria zitaanza kuchukuliwa dhidi yao.
‘’Wapo walioikopa na kusababisha benki hiyo ikafilisiwa hadi ikafungwa fedha hizo lazima
zirudi nimefatilia nimeona wako watendaji wanaendelea na maisha kama kawaida
zimo taasisi zinaedelea na maisha kama kawaida huku fedha zilizokuwa za wakulima hazieleweki zilipo’’alisema Brigedia
Gaguti.
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa amewataka viongozi
wa vyama hiyo kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja
wanapmatia taarifa kuhusu namna ya rasilimali za vyama hivyo
zinavytumika na namna zinavyowanufaisha wakulima .
No comments:
Post a Comment