Na Asha Mwakyonde
SERIKALI imesema kuwa inatarajia Bunge kupitisha mapendekezo
ya mabadiliko ya sheria ili watu waweze kujipima wenyewe virusi vya ukimwi
mwishoni mwa wiki hii.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akifungua semina elekezi ya Virusi Vya Ukimwi
(VVU), kwa wasanii mbalimbali iliyoandaliwa na wizara hiyo kwa kushirikiana na
Taasisi ya Benjamin William Mkapa.
Waziri Ummy alisema awali Sheria ilikuwa hairuhusu kujipima na kwamba
kwa sasa itakuwa rasmi kabla ya ijumaa hivyo sheria hiyo ikipita sasa watu
wataweza kujipima wenyewe.
Alisema yamepelekwa bungeni marekebisho hayo ya sheria ili
watu waweze kujipima wenyewe. lakini pia sheria ya ukimwi inasema mtoto mwenye
umri wa chini ya miaka 18 hawezi kwenda kupima ukimwi bila ridhaa ya wazazi.
“Kujipima virusi vya ukimwi sio kipimo cha mwisho tutakuomba uende
kwenye kituo cha kutoa huduma za afya ili uweze kuthibitisha kama ni sahihi au
sio sahihi,” alisema Waziri Ummy.
“Watoto ni watundu hivyo tumepeleka mapendekezo
bungeni Vijana wa miaka 16 na 17 hawezi kupima mpaka mama au mzazi aandike apime,tumeona watoto
wanaendelea wana access na mitandao tumepeleka pia mapendekezo hayo bungeni naamini ijumaa wabunge watapitisha
mapendekezo yetu,”alisema.
Waziri Ummy alisema kuwa kutokana na hali hiyo wizara
yake hadi mwenye umri wa miaka 15
kwenda kupimwa kwenye vitu na kwamba serikali
imeendelea kuwatumia wasanii katika shughuli mbalimbali kwa lengo la kuhamasisha vijana kujitamu
kuhusu sula la maambukizi ya vvu na ukimwi.
“Lakini si kwa kiwango kinachotakiwa kwa kuwa wasanii wana ushawishi
mkubwa wa kufikisha ujumbe kirahisi na kwa haraka kwa vijana ama washabiki wao,”alisema.
Waziri Ummy aliongeza kuwa kila watanzania 100, watanzania 80
wanafahamu kuhusu virusi vya ukimwi na ukimwi.
Alieleza kuwa Tanzania imejiwekea malengo ya kutokomeza ukimwi
ifikapo 2030 na kwamba watu Mil 1.4 nchini wanaishi na virusi vya ukimwi angalao
asilimia 90 wafahamu kuhusu hali zao hiii ndiyo imekuwa changamot kubwa.
“Nawaomba sana katika kazi zenu za Sanaa kwenye nyimbo maigizo
filamu Sanaa za maonyesho katika kuhamasishana. Kwani Katika watu 100 wanaoishi
na virusi vya ukimwi ni watu 62 tanzania ambao wanafahamu kuhusu hali zao katika
maambukizi,”alisema.
Aliongeza kuwa kuwa kuna asilimia 38 katika ya watu 100 wanaoishi na
virusi vya ukimwi hawajaweza kuwafikia
na kwamba watu wanaoishi na virusi vya ukimwi na wanajua hali zao wawe
wanatumia dawa za ARVs.
“Kuna utafiti na ushahidi wa kisayansi unapotumia ARVs kwa
kuzingatia masharti uwezo wa kuambukiza unapungua kwa zaidi ya asilimia 645 na
asiyetumia ARVs ana nafasi ya kuambukiza watu wengi kuliko yule anayetumia,”alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji katika taasisi hiyo ya
Benjamini William Mkapa, Dk. Ellen Senkoro alisema Hivyo wasanii ni kundi
muhimu linaloweza kusaidia kufikia vijana kwa ukaribu.
Aliongeza kuwa taasisi hiyo inatambua vijana ni kundi mojawapo
linalokabiliana na vishawishi vingi vinavyosababisha maambukizi ya ukimwi.
Alisema semina hiyo
wanawajengea uwezo wasanii kufikisha ujumbe jinsi inavyotakiwa kwa kuwa ni
washawishi wazuri kwa lengo la kuhakikisha wanapunguza kasi ya maambukizi ,
unyanyapaa na kuhimiza matumizi sahihi ya dawa za kupunguza makali ya virusi
vya ukimwi.
Awali Mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Yudas Ndungile
alisema wizara ya afya imepiga imejitahidi kuhakikisha inatoa elimu ya vvu kwa
kupitia Sanaa.
Wasanii hawa watapitishwa kwenye athari za unyanyapaa, na kupitia
Sanaa inaweza kutumika kufikisha ujumbe
kwa jamii juu ya kujikinga na maambukizi, kutumia dawa, jinsi ya kuepuka madawa
ya kulevya lakini pia namna ya kuondokana na unyanyapaa.
Naye Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Addo Novemba
alisema, imekuwa ni desturi kwa wasanii kutangulizwa kufanya jambo hivyo
wanaiomba wizara nyingine waige mfano huo kwa kuwa wanafanya kazi kubwa ya
kuielimisha jamii.
Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Sanaa za Maonyesho,
William Chitanda alisema wasanii wapo tayari kushirikiana na wizara kuhakikisha
Sanaa zao zinapeleka ujumbe muafaka.
No comments:
Post a Comment