Mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere (kushoto), akimtoka beki wa Tanzania prisons, vedastus mwihambi, katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. (Picha na John Dande).
Winga wa Simba, Clatous Chama (kushoto), akitafuta mbinu zakumtoka Tanzania Prisons, Vedastus Mwihambi, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Kikosi cha Simba.
Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' akitoka kushuhudia pambano la Simba na Tanzania Prisons.
NA JOHN MARWA
MABINGWA watetezi Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) Simba SC wameshindwa kutamba na kuambulia pointi moja dhidi ya Tanzania Prisons 'Wanajelajela' mchezo wa VPL uliotandazwa leo Novemba 7, 2019 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Simba na Prisons ziliumana na kutoshana nguvu kwa pambano lao kumalizika kwa suluhu.
Simba waliingia kwenye kipute hicho wakitoka kupata ushindi mnono mchezo wa mwisho dhidi ya Mbeya City kwa mabao 4-0.
Wakati Prisons waliingia kwenye mechi hiyo wakiwa hawajapoteza mchezo kwenye Ligi msimu huu na kufanikiwa kuendeleza rekodi yao ya kuwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo hadi sasa.
Kwa matokeo hayo Simba wanasalia kileleni na pointi 22 za michezo tisa wakishinda mechi saba sare moja na kupoteza moja.
Ligi hiyo itaendelea kesho mwa Yanga kukwatuana na Ndanda FC wanakuchele Dimba la Nagwanda Sijaona mjini Mtwara.

No comments:
Post a Comment